Malala Yousafzai,
Madaktari nchini Pakistan wamefanikiwa kutoa risasi kichwani mwa msichana wa miaka 14 mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel, Malala Yousafzai.
Hii ni baada ya msichana huyo kushambuliwa kwa kupigwa risasi hapo jana alipokuwa akitoka shuleni Kaskazini Magharibu mwa eneo la Swat.
Taarifa kutoka kwa madakatari wake zinaeleza kuwa hali ya msichana huyo iko shwari kwa sasa.
Malala alituzwa tuzo la nobel kutokana na juhudi zake za kupigania haki ya elimu kwa wasichana wa Taliban ambao kwa mujibu wa desturi za kitaliban haswa katika eneo la Swat walikuwa hawaruhisiwi kupata elimu
Ndugu yake aliambia BBC kuwa, madaktari,wangali wanatafakari ikiwa wampeleke nje kwa matibabu zaidi.
Kundi la Taliban lilisema lilihusika na shambulizi hilo.
Malala Yousafzai aliandika kitabu cha kumbukumbu zake binafsi kwa niaba ya BBC miaka mitatu iliyopita wakati eneo la Swat lilikuwa linadhibitiwa na kundi laTaliban.
Wanasiasa nchini Pakistan, walilaani shambulizi hilo huku Marekani ikilitaja kama kitendo cha uoga
1 comment:
propaganda dhidi ya uislamu lakini uislamu umesimama imara na wala hatokufa leo wala kesho kwa sababu mungu ndo anaye ulinda dunia nzima wana propaganda dhidi ya uislamu wanadhani wataukashifu na kuuharibu na kuuuwa watu wachukie wasiingia katika dini hii au walio wa dini hii waone haya but no its outshine them all the time and always and forever.
nimeandika hayo kwa sababu kuna research kibao zinaonyesha njama hizi za propaganda zenu na pia kuna sehemu ambazo kwamba kuna idadi ya wakiristo hawajui kusoma wala kuandika na wanafuata mila zao na watoto wa kike wanakaa nyumbani kusubiri kuolewa.
madrasa daima ndo inayomfunza na kumkuza muislamu wa jinsi zote vizuri sana kuliko elimu ya dunia ambao inamfudisha uwizi na kila ufisadi na jinsi ya kuwa fisadi katika dunia hiii
Post a Comment