UNAFAHAMU nini juu ya upweke? Unavyojua wewe ni nini? Bila shaka kila mmoja ana jibu lake. Ni ukiwa...kunyong’onyea au kubaki katika wakati mgumu kutokana na jambo fulani. Kwa kuwa hapa kwenye All About Love, tumeegemea zaidi kwenye mapenzi, bila shaka upweke ninaouzungumzia hapa, wengi wetu wanauelewa.
Tutajadili juu ya kuushinda upweke katika moyo wako. Natambua kuna baadhi ya wanawake au wanaume wanakaa kipindi kirefu bila ya kutamkiwa kuwa wanapedwa, kutokana na hali hiyo wanakuwa wapweke na wakati mwingine kufikiria kuwa wao ni wabaya na wasiostahili kabisa kuwa na wapenzi.
Tutajadili juu ya kuushinda upweke katika moyo wako. Natambua kuna baadhi ya wanawake au wanaume wanakaa kipindi kirefu bila ya kutamkiwa kuwa wanapedwa, kutokana na hali hiyo wanakuwa wapweke na wakati mwingine kufikiria kuwa wao ni wabaya na wasiostahili kabisa kuwa na wapenzi.
Wengine huanza kujiona hawafai kutokana na sababu ambazo wenyewe wataziweka ambazo kwa kiasi kikubwa huwa za kujikosoa wao wenyewe.
Wakati mwingine huanza kufikiria kuwa huenda kwa sababu yupo katika hali fulani ndio maana hapati mtu wa kumpenda na fikra nyingine mbaya juu yake ambazo huwa ni za kujikatisha tamaa.
Tambua kitu kimoja, kuna wasichana warembo na wavulana watanashati wengi ambao hawajapata pumziko la kweli katika mioyo yao kwa muda mrefu sasa, wamekuwa wakitafuta watu wenye mapenzi ya kweli kwa muda mrefu bila mafanikio na sasa wamekata tamaa ya kupata wapenzi wa kweli na badala yake wamegeuka vyombo vya starehe.
Wavulana watanashati au wasichana warembo mara nyingi watu wa upande wa pili huwatamani zaidi kuliko kuwa na mapenzi ya kweli, kwa maana hiyo baada ya kushiriki naye ngono mara kadhaa huamua kuachana naye na kumuacha muhusika akiwa na sononeko katika moyo wake.
Ndiyo upweke ninaouzungumzia hapa.
Watu wa aina hii huachwa na dhiki ya moyo na wakati mwingine hukata tamaa na kuamua kutokuwa na uhusiano mwingine kabisa na wapenzi wapya. Jaribu kufikiri kama kuna mtu wa aina hii ambaye amekuwa akitoneshwa mara kadhaa na wapenzi na wewe ambaye una miezi karibu sita sasa hujapata akupendaye nani mwenye matatizo zaidi? Nadhani jibu yakinifu utakuwa nalo.
Inawezekana wewe ni mmoja kati ya hao ambao wana sononeko la moyo kwa kutopata faraja ya kweli kwa wapenzi wao. Hakika hizi ni mada mbili tofauti lakini leo nitaanza na hili la kutopata mpenzi kwa muda mrefu na sasa umekata tamaa ya kupedwa, kuoa au kuolewa katika siku zote za maisha yako.
Wakati mwingine inawezekana hujafahamu chanzo cha wewe kutopata mpenzi, lakini kuna mambo mengi ya kuzingatia ili uweze kupata mpenzi na hivyo kuepuka upweke katika moyo wako.
KWANZA JIJALI...
Inawezekana ukawa na maswali lukuki kutokana na kipengele hicho hapo juu. Je, unajijali? Nataka utambue kitu kimoja, kuwa kuna baadhi ya watu hawajipendi! Hivi unadhani kama wewe mwenyewe hujipendi, hujithamini nani atakupenda?
Ninaposema ujipende namaanisha ujipe upendo ule wa kawaida wewe mwenyewe kabla ya kuhitaji upendo wa mtu mwingine. Mwingine anaweza akawa anavaa nguo chafu, hapigi pasi, nywele zipo timtim nani atakupenda kwa misingi hiyo?
Hakuna anayependa kuwa na mtu ambaye hana desturi ya usafi kwanza hata kama ni mzuri kisi gani unapokuwa upo rafu sana hakuna mtu ambaye atausumbua moyo wake kuanza eti kukufikiria wewe usiyejipenda.
Sio lazima wakati wote uwe ‘smart’, kwa kuwa inawezekana wengine wanafanya kazi ngumu ambazo mazingira yake lazima wanakuwa katika hali ya uchafu, lakini baada ya kazi unapaswa kuwa msafi kabisa mbele za watu.
Upande wa wasichana sio lazima uweke nywele zako dawa au usuke rasta wakati vitu hivyo huna uwezo navyo, unaweza ukasuka nywele zako vizuri au wakati mwingine ukanyoa mtindo mzuri unaokubalika ambao hautakutafsirisha vibaya kwa jamii.
Anza kujipenda kabla ya kuhitaji upendo kutoka kwa mtu mwingine, hiyo itakusaidia kuwa na mvuto na mwonekano mzuri kiasi cha kuweza kumpagawisha mtu mwingine kuanza kuhisi cheche za moto wa mapenzi katika moyo wake.
Bado mada inaendelea. Usikose wiki ijayo.
Joseph Shaluwa ni Mshauri wa Mambo ya Mapenzi anayeandikia magazeti ya Global Publishers, ameandika vitabu vya True Love, Let’s Talk About Love na All About Love vilivyopo mitaani.
1 comment:
nakubali sana hii topi yamenikuna mimi binafsi ndo maana nakubali sana nilikuwa sijipendi eti siyo kwamba niko mchafu nilikuwa nako smart kila wakati lakini ninachozungumzia mimi hapa ni kwamba nilikuwa nawajali sana wenzangu mtu akipatwa na shida wakwanza mimi kufuata hata kama si rafiki yangu au mtu wakaribu au hata kama simjui nikiwa kituo cha basi nikimuona mama au hata kaka anasononeka huwa namfariji kwa maneno mazuri asikate tamaa, na akiwa rafiki yangu ndo kabisa nayacha yangu nayafuata yake kumsadia kwa kila hali japo kuwa sina uwezo wa kipesa lakini nimekuja kugundua nikipata mimi matatizo huwa sina tabia ya kuyazungumza lakin mtu anaweza kunihisi basi hata msada wa maneno matamu siyapati kutoka kwa hao marafiki
so nikaaza kubadili mawazo yangu nikaaza kujijali mwenyewe na kufanya vyangu na hata kama mtu aje na machozi ya damu debe lijaye kama sijayafanya yangu simfuati wala kumsikiliza yake kwa sababu wao wanafanya yao mimi hakuna wakunifanyia yangu na ninashida zangu na mimi pia ndo maana hivi sasa najipenda mimi and only me first,i come first before anybody else in this world
sasa watu wananiona nime badilika na nimekuwa SELFISH BUT I DONT CARE I DONT CARE NIPO KATIKA ZARI YANGU, Najua duniani kuhurumiana na kusaidiana lakin ukiwa na upendo mkubwa kama nilivyokuwa nao hapo zamani unaonekana mjinga na fara na watu watakutumia so jipendeni wenyewe kwanza halafu wenginewe.
sometimes najua nakosea lakin naona niendapo ndo pazuri no more headache za kujali ya watu,lakin anaye nijali na mimi nitamjali kwa hali na mali
Post a Comment