ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, October 10, 2012

WAREMBO WA REDD'S MISS TANZANIA 2012 WAKUTANA NA MH. LOWASSA MONDULI


Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akisalimia na Msimamizi (Matron) wa warembo wa Redd's Miss Tanzania 2012,Irene Karugaba wakati Warembo hao walipotembelea Nyumbani kwa Waziri Mkuu Mstaafu,Monduli ili Kupata Baraka zake.Mh. Lowassa aliwapokea warembo hao kwa furaha na kuzungumza nao machache juu ya mafanikio ya Mashindano hayo na Maendeleo ya Taifa letu la Tanzania.
Picha juu na chini Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akizungumza na Warembo wanaowania Taji la Redd's Miss Tanzania 2012 waliofika nyumbani kwake Monduli leo na kupata wasaa kwa kuzungumza nae mambo mawili matatu juu ya mafanikio ya Mashindano hayo na Maendeleo ya Taifa letu kwa ujumla.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa na Mkewe Mama Regina Lowassa wakiwa kenye picha ya pamoja na Warembo wanaowania Taji la Redd's Miss Tanzania 2012 pamoja na Viongozi wa Kamati ya Miss Tanzania.
(Picha Zote kwa Hisani ya Intellectuals Communications Limited

1 comment:

Anonymous said...

upuzi mtupu eti warembeo wanamtembelea mheshimiwa nyumbani kwake kwa baraka mmeona hii kitu ime kaa sawa, badala ya kwenda mbele kielimu eti leo tunakwenda katika sana za urembo na uimbaji na movies etc mbona hatuoni watafiti wa kisayansi watanzania wanawake wakufunzi wakifanya haya kwa sababu hatunao kila kukicha mambo ya ma miss miss na starehe kwenda mbele za kipuuzi kuwapotosha vijana wetu especially watoto wa kike

inauma sana mimi kama mzazi nasikitika sana taifa letu liendapo na jinsi tunavyowakuza watoto wetu wa kike

shule ndo muhimu siyo sana hizi zinazo wafundisha watoto mabalaaa