Mchungaji Perucy Butiku akiongoza Ibada ya kumuombea Marehemu Jesca Emmnauel na kuwafariji wazazi wake, ambapo pia alitumia fursa hiyo kuwakumbusha waombolezaji kwamba kila mmoja wetu anasiku yake atakayoitwa na Mwenyenzi Mungu, kama alivyoitwa Mtoto Jesca, ni siku ambayo hakuna mtu aijuaye. Na kwa sababu hiyo akasisitiza umuhimu wa kujiandaa. Ibada ilifanyika siku ya Jumamosi Bergen Funeral Home jijini New York.
Mama mzazi wa Jesca Bi. Doto akilia kwa uchungu mara baada ya kuona mwili wa mtoto wake.
Baba mzazi wa Jesca, Bw. Emmanuel akilia kwa uchungu mara baada ya kumwona mtoto wake, pembeni yake ni Shangazi wa Jesca, Bi. Rose
Mdogo wake Jesca, Catherine akiwa ameelemewa na majonzi mazito kwa kuondokewa na dadayake, Catherine aliwatia uchungu waombelezaji pale alipomuaga Dada yake kwa kutamka " Bye Jesca".
Naibu Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi akimuaga Jesca
Brigedia Jenerali Maganga Mwambata Jeshi katika Ubalozi wa Tanzania nchi Marekani, akiaga. Brigedia Jenerali Maganga ni kati ya Maafisa wanne waliowakilisha wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani.
Balozi Tuvako Manongi akiungana na waombelezaji wengine kumuaga marehemu Jesca. Baada ya ratiba ya kuaga, Balozi Manongi aliwashukuru watanzania kwa ushirikiano, upendo na mshikamano mkubwa waliouonyesha wakati wote wa kipindi cha maombolezo ya msiba huo na akawasihi kuendeleza umoja huo
Bw. Emmanuel na Bi. Doto wakiwa na mtoto wao, muda mfupi kabla ya sanduku kufungwa
Sanduku lenye mwili wa Jesca tayari kwa Safari ya kwenda Bumbombi- Tarime Tanzania kwa Mazishi.
Watanzania wanaoishi jijini New York na Vitongoji vyake wakiwamo wawakilishi kutoka Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, jana Jumamosi, waliungana na Familia ya Bw. Emmanuel Alfred Swere na Bi. Doto na wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, katika Ibada ya kumuaga Jesca Emmanuel (12) aliyefariki ghafla Jumapili iliyopita.
Ibada ya kumuaga Jesca ilifanyika Bergen Funeral Home na iliongozwa na Mchungaji Perucy Butiku. Mazishi ya Marehemu Jesca yanatarajiwa kufanyika siku ya Jumanne katika kijiji cha Bumbombi- Tarime Tanzania.
Ibada ya kumuaga Jesca ilifanyika Bergen Funeral Home na iliongozwa na Mchungaji Perucy Butiku. Mazishi ya Marehemu Jesca yanatarajiwa kufanyika siku ya Jumanne katika kijiji cha Bumbombi- Tarime Tanzania.
Raha ya Milele Umpe Eee Bwana na Mwanga wa Milele Umuangazie Apumzike kwa Amani. Amina
No comments:
Post a Comment