ANGALIA LIVE NEWS

Friday, November 23, 2012

PITA PITA YA VIJIMAMBO THANKSGIVING NYC

Pita pita ya vijimambo thanksgiving NY hapa ni DJ bora kabisa NYC, DJ Bilal akiwarusha wabongo ndani ya house party ya thanksgiving iliyofanyika nyumbani kwa Fundikombo Valley Stream Long Island, NY. Watu walienjoy music kutoka kwa Dj Bilal baada ya kutanguliwa na chakula kilichokuwa kimeandaliwa na Fundikombo na mama mwenye nyumba wake. Chini ni picha ya matukio yaliyojiri katika house bush party hiyo.
 Katika Bush hiyo ya ndani palikuwa na vinywaji vyote na vilipatikana bure kama unavyoona konyagi, kilimanjaro na serengeti bia zilikuwepo ili kuwapatia wapenzi kitu roho inapenda. Kwa roho safi brother Fundikombo alitoa huduma hiyo bure kukitanguliwa na chakula.
 Watu wakipata kitu cha mduara taratibu bila jasho 
 Palikuwa apatoshi kwani kila mtu hakuweza kujizuia kucheza kila kibao kilichorushwa hewani na DJ Bilal.
 Ilikuwa furaha kwa watu wote waliojitokeza katika house party hii kwani watanzania wa NY huwa hatukutani mara kwa mara, hivyo tunavyopata nafasi kama hii inapendeza watu kuenjoy kwa music wa kinyumbani kutoka kwa maDj wetu. Dj Dave, Dj Mao na Dj Bilal.
 Miss. Lydia akiwa na baba mwenye nyumba wake na binti yao katikati wakipata ukodak wa vijimambo katika house party hiyo ya thanksgiving nyumbani kwa Fundikombo.
 Brother Fundikombo na mama mwenye nyumba wake katikati wakipata ukodak mbele ya camera ya vijimambo. Kwa picha zaidi bofya read more.

Ma Dj wakipata ukodak Dj Mao na Dj Fundikombo

No comments: