ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, November 24, 2012

RATIBA YA KUMUAGA MAREHEMU JESCA EMMANUEL



Mhe. Tuvako Manongi, Balozi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, anawataarifu watanzania wanaoishi Jijini New York na Vitongoji vyake kwamba, Marehemu Jesca Emmanuel (12) aliyefariki ghafla Jumapili iliyopita ataagwa rasmi siku ya Jumamosi tarehe 24/11/2012.

Mahali ni :Bergen Funeral Service Inc,
114-30 Rockaway BLVD,
So, Ozone Park, NY 11420
Simu:718-738-8383
www. Bergenfuneral.com

Muda: Kuanzia saa Tatu Asubuhi (9.00am) hadi saa Sita Mchana ( 12.00 noon)

Tafadhali tunaombwa sana kuzingatia muda, baada ya ratiba ya kumuuga Mpendwa wetu Jesca Emmanuel kukamilika, mwili wa marehemu ukisindikizwa na wazazi wake utaondoka usiku wa siku hiyo ya Jumamosi kwa safari ya Bumbombi- Shirati Tanzania kwa mazishi.

“Jesca, wazazi wako, mdogo wako, shangazi yako, rafiki zako wanafunzi wenzako na sisi sote tuliokufahamu tulikupenda sana. Lakini Mwenye-Enzi Mungu amekupenda zaidi. Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe. Amina”

Raha ya Milele Umpe Eee Bwana na Mwanga wa Milele Umuangazie apumzike kwa amani. Amina.

UBALOZI WA TANZANIA UMOJA WA MATAIFA

NEW YORK

No comments: