ANGALIA LIVE NEWS

Friday, November 23, 2012

SAJUKI KUWAMWAGIA SHUKURANI LIVE KWA MARA YA KWANZA IRINGA


KATIKA kutoa shukrani kwa Watanzania wote waliowajibika katika kuhakikisha wanamsaidia mwigizaji na mtayarishaji mahiri wa filamu kutoka Swahiliwood Juma Kilowoko ‘Sajuki’ kupatiwa matibabu kutokana na maradhi ya tumbo na kwenda kutibiwa Nchini India na kupona, kampuni ya Wajey Film Company imeandaa tamasha kubwa la shukrani.

Ni tamasha la aina yake kutokana wa wadau wafilamu na Watanzania kwa ujumla kufurahia kurudi kwa sajuki katika hali yake ya mwanzo, Stara alisema onyesho hilo litafanyika kwa ajili ya kukusanya fedha zitakazopelekwa kwa wasanii wanaosumbuliwa na maradhi na kukosa matibabu alisisitiza mratibu huyo.

Bongo5 iliongea na mmoja wa wakurugenzi wa kampuni hiyo mahiri katika utengenezaji wa filamu, Wastara Juma ‘Stara’ amesema kuwa baada ya mumewe Sajuki kupata matibabu anatumia fursa hiyo katika kuwashukru watanzania waliojitoa kwa hali na mali katika kufanikisha matibabu hayo.

kama familia hatuna cha kuwalipa watanzania kwa moyo wao wa upendo walioonyesha kwetu, katika kipindi kigumu na majaribu wakati Sajuki akiwa anaugua, si rahisi kumfikia kila mtu kwa wakati mmoja lakini kwa njia ya tamasha hilo tutawafikia, tunawapenda watanzania mungu awabariki sana,”anasema Wastara.

Tamasha hilo linatarajia kufanyika siku ya jumapili Tarehe 25/11/2012 katika uwanja wa Samora huku wasanii wa muziki wakitumbuiza kwa nguvu Mzee Yusuf, Linah, H. Baba na mchekeshaji Kitale ataimba burudani kubwa ni pale mechi kali itakapopigwa kati ya wasanii nyota wa filamu kutoka Bongo movie na timu kali ya watangazaji wa redio zote mkoani Iringa.

No comments: