Askari wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wakitoa heshima kwa mwendo wa pole mbele ya Luteni Jenerali Mstaafu A Shimbo (hayupo pichani) wakati wa sherehe za kumuaga zilizofanyika leo katika kambi ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Mgulani jijini Dar es Salaam. Luteni Jenerali Mstaafu Shimbo amelitumikia jeshi hilo kwa zaidi ya miaka 41 kwa kushika nyadhifa mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na mnadhimu mkuu wa Jeshi.
Mkuu wa Majeshi ya ulinzi nchini Jenerali Davis Mwamnyange akimkabidhi hati ya utumishi Luteni Jenerali Mstaafu Abdulrahman Shimbo (kushoto) wakati wa sherehe za kumuaga zilizofanyika leo katika kambi ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Mgulani jijini Dar es Salaam. Luteni Jenerali Mstaafu Shimbo amelitumikia jeshi hilo kwa zaidi ya miaka 41 kwa kushika nyadhifa mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na mnadhimu mkuu wa Jeshi.
Baadhi ya askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakiangalia gwaride la sherehe za kumuaga Luteni Jenerali Mstaafu Abdulrahman Shimbo (hayupo pichani) zilizofanyika leo katika kambi ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Mgulani jijini Dar es Salaam.
Luteni Jenerali Mstaafu Abdulrahman Shimbo akikagua kikosi cha askari wa kike kutoka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakati wa sherehe za kumuaga rasmi zilizofanyika leo katika kambi ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Mgulani jijini Dar es Salaam. Luteni Jenerali Mstaafu Shimbo amelitumikia jeshi hilo kwa zaidi ya miaka 41 kwa kushika nyadhifa mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na mnadhimu mkuu wa Jeshi.
Ndugu, jamaa na marafiki wa Luteni Jenerali Mstaafu Abdulrahman Shimbo (wan ne mstari wa mbele kulia) wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa sherehe za kumuaga zilizofanyika leo katika kambi ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Mgulani jijini Dar es Salaam.Wa katikati mstari wa mbele ni Mkuu wa Majeshi ya ulinzi nchini Jenerali Davis Mwamnyange.
Picha na Anna Nkinda – Maelezo
No comments:
Post a Comment