Miili ya wanafunzi wa shule ya msingi imezu ikichukuliwa na wanausalama watoto hao walikuwa wakivuka barabara akielekea shuleni ndipo roli hilo lilipowagonga na kukimbia huku miili ya watoto hao ikiwa imetawanyika vipandevipande ajali hiyo imetokea mida ya saa moja na nusu asubuhi
Watoto hao wamegongwa katika barabara kuu itokayo Zambia kwenda dsm maeneo ya imezu inyara wilaya ya mbeya vijijini
Waanchi kwa hasira wameamua kufunga barabara hiyo wakimtaka mkuu wa mkoa mbeya aje afike eneo la tukio wamweleze kero zao za barabara hiyo kwani sasa inawamaliza wanakijiji hao kwa ajali za mara kwa mara katika eneo hilo
Vijana wameshaanza kuweka mawe barabarani kuzuia magari yasipite na ukizingatia hii ndiyo barabara kuu ya magari yaendayo Malawi na zambia na mikoa ya jirani
Habari kamili tutawaletea baadae mpaka tunaondoka eneo la tukio mkuu wa mkoa Mbeya bado hajafika eneo la tukio na habari zisizo rasmi dereva aliyewagonga watoto hao kajisalimisha katika kituo cha polisi Inyala
Picha habari na Mbeya yetu
No comments:
Post a Comment