Rais Kikwete na Zitto Kabwe
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe amefichua siri ya uhusiano wake na Rais Jakaya Kikwete kuwa, unatokana na kuheshimu mchango wake anaoutoa kwa taifa.
Kutokana heshima hiyo, Zitto anasema ndiyo maana Rais Kikwete hakufika jimboni kwake katika uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2005 na mwaka 2010 kumnadi mgombe wa CCM.
Zitto ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema alisema hayo katika mahojiano maalum na Mtandao wa Jamii Forum juzi.
Mbunge huyo ambaye pia ni Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni, jana alilithibitishia gazeti hili kwamba alihojiwa na mtandao huo kwa saa nane.
“Kweli ni mahojiano baina yangu na Jamii Forum. Kwa Kfupi ni kwamba, yalikuwa mahojiano ya saa nane, kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa kumi jioni na walionihoji kwa njia ya mtandao walikuwa wakituma maswali na mimi nawajibu,” alisema Zitto.
Alisema yeye na Rais Kikwete wana uhusiano nje ya siasa na hata siku moja hawajadili mambo ya vyama vyao wanapokutana na kwamba, Rais anaamini katika uzalendo wake.
Zitto alisema kutokana Rais Kikwete kuthamini mchango wake, ndiyo maana hajawahi kwenda kwenye jimbo lake kumfanyia kampeni mgombea wa chama chake cha CCM katika chaguzi za mwaka 2005 na 2010.
“Hatuna makubaliano yeyote, bali anaheshimu mchango wangu kwenye nchi yangu. Mwaka 2005 hakuja Kigoma Kaskazini na 2010 pia hakuja Kigoma Kaskazini,” alisema.
Alisema kama ilivyo kwa wengine wenye uamuzi ya kuthamini kazi za wagombea wa vyama vingine, Rais Kikwete naye anayo haki ya kuheshimu na kuthamini kazi zake.
Alisema kama ilivyo kwa wengine wenye uamuzi ya kuthamini kazi za wagombea wa vyama vingine, Rais Kikwete naye anayo haki ya kuheshimu na kuthamini kazi zake.
Aithdha, Zitto alisema anamheshimu Rais Kikwete kama mzee wake na kwamba, kuwaita kuwa wao ni marafiki ni kukosea.
“Kuita sisi ni marafiki ‘is understatement’, yeye ni mzee wangu. Tunaheshimiana, lakini ninaiheshimu zaidi Tanzania na ninaipenda zaidi Tanzania,” Zitto alisema.
Alichokifanya Rais Kikwete kutokuja katika jumbo langu si jambo geni, kwani hata vyama vingine vimewahi kuvifanya.
Alitoa mfano wa aliyekuwa mgombea wa urais kupitia Chadema katika uchaguzi mkuu mwaka 2005, Freeman Mbowe alipofika katika Jimbo la Musoma Mjini, alimpigia kampeni mgombea wa CUF.
Zitto alikumbusha kuwa na katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, aliyekuwa mgombea wa urais wa chama chake, Dk Willibrod Slaa alipofika jimbo la Kyela alimnadi mgombea wa CCM, Dk Harrison Mwakyembe kutokana na kutambua na kuheshimu mchango wake kwa taifa.
Uhusiano wa CCM
Kuhusu watu wanaomhusisha na CCM, mwanasiasa huyo alisema kuna kikundi kidogo cha watu wenye malengo mabaya dhidi yake ndio wanaoeneza uvumi huo.
Uhusiano wa CCM
Kuhusu watu wanaomhusisha na CCM, mwanasiasa huyo alisema kuna kikundi kidogo cha watu wenye malengo mabaya dhidi yake ndio wanaoeneza uvumi huo.
“Wajue tu kwamba, hawawezi kuwadanganya Watanzania ambao wanafanya uamuzi wao si kutokana na propaganda, ila kutokana na matendo ya kila mmoja,” alisema.
Aliwaonya watu hao kuwa, hawawezi kummaliza yeye kisiasa bila kuiathiri Chadema kwani taswira yake imefungana na chama hicho.
Alisema: “Wanaoeneza sumu hiyo hawana nia njema na Chadema. Hawaelewi siasa. Maadui wanawachochea kwa kuwapa habari za uwongo na wao wanadhani watammaliza Zitto. Huwezi kummaliza Zitto bila kuiathiri Chadema. Hawatafanikiwa,”.
Kuhusu kuwapo kwa utitiri wa vyama vya siasa nchini, Zitto alisema watu waachiwe kuanzisha vyama waanvyotaka, lakini baadaye vitajichuja na kubaki vyama viwili vyenye nguvu; Chadema na CCM.
Alisema vyama vitakavyobaki ni vile ambavyo vitakidhi matakwa ya wananchi na kwamba, hakuna haja ya kuweka sheria ya kuvifuta vyama vingine.
Zitto aliitabiria mabaya chama cha NCCR Mageuzi, akisema haoni kama kitaweza kitaendelea kuwapo.
Aliongeza kuwa, UDP hakiwezi kuwapo bila ya Mwenyekiti wake, John Cheyo na TLP hakiwezi kuwapo bila ya Mwenyekiti wake, Augustine Mrema.
“Sioni NCCR ikidumu. Sioni future (tumaini) ya UDP bila Cheyo na TLP bila Mrema,” alisema.
Hata hivyo, alisema kuna uwezekano CCM kumeguka na kundi kubwa litakalotokana na tukio hilo likaunda chama kingine cha siasa ambacho kinaweza kuwa na nguvu zaidi hata ya Chadema.
Alisema baada ya uchaguzi wa 2015 tutaona mambo haya. “Tuache watu wawe huru kuunda vyama na vyenye nguvu vitabakia,”
Kuhusu tetesi kuwa amenzisha chama na Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila, Zitto alisema hajawahi na wala hafikirii kuanzisha chama cha siasa.
Alisema chake chake ni Chadema na hataondoka kwenda chama kingine cha siasa na kushangaa kuona baadhi ya viongozi wa Chadema wanaamini uongo huo.
“Kinachonisikitisha ni kwamba, kuna viongozi wa Chadema wamekula sumu hii na bila woga wanaisema kana kwamba ni kweli,” alisema
Ubunge wake
Zitto alirejea kauli yake aliyowahi kuitoa kwamba hatagombea ubunge katika jimbo la Kigoma Kaskazini na badala yake anataka kugombea urais kupitia cha hicho mwaka 2015.
Alisema ametangaza kutogombea ubunge, na anakiomba ridhaa ya chama chake kuwa mgombea urais na kuwa, hilo lisipowezekana atakuwa mpiga debe wa mgombea Urais.
Zitto alirejea kauli yake aliyowahi kuitoa kwamba hatagombea ubunge katika jimbo la Kigoma Kaskazini na badala yake anataka kugombea urais kupitia cha hicho mwaka 2015.
Alisema ametangaza kutogombea ubunge, na anakiomba ridhaa ya chama chake kuwa mgombea urais na kuwa, hilo lisipowezekana atakuwa mpiga debe wa mgombea Urais.
Alisema hataki itokee yaliyotokea mwaka 2010 ambapo mgombea Urais alibaki mpweke kwani kila mtu alikwenda kugombea Ubunge.
Zitto alifafanua kwamba, Chadema kina viongozi wengi wanaoweza kupewa uongozi wa nchi na aliwataja baadhi yao kuwa ni Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, Katibu Mkuu Dk Slaa na mmoja wa makada wa Chadema, Dk Kitila Mkumbo.
“Wapo wengi sana ndani ya CHADEMA wenye sifa za kuwa Marais. Sina mashaka kabisa hilo,” alisisitiza.
Aliongeza kuwa, ili Tanzania iwe salama ni lazima CCM ishindwe uchaguzi mkuu ujao.
Alibashiri kuwa, kama CCM kitashinda tena mwaka 2015, watu wengi hasa wanamageuzi watavunjika moyo na wengine wanaweza kabisa kukata tama.
“Njia pekee ya kuisadia CCM ili iweze kujipanga upya ni chenyewe kondoka madarakani. Chadema tuna nafasi kubwa ya kushinda na kuongoza dola. Muhimu chama kijipange na kuonekana kama chama kilicho tayari kushika dola. Tuyatende tunayoyasema na tujiimarishe zaidi,” alisema Zitto.
Kuhusu demokrasia ndani ya Chadema, Zitto alisema chama hicho kina demokrasia ya aina yake na wanachama wanaridhika nayo.
“Tuna utaratibu mzuri sana wa kujieleza na kutetea hoja zetu ndani ya chama na baada ya watu wote kukubaliana tunahakikisha tunasimama wote kwa kauli moja sehemu zote tunapokiwakilisha chama. Sio katika kupanga safu za uongozi tu, bali katika maeneo yote,”alisema.
Mwananchi
No comments:
Post a Comment