Waziri wa Nishati na Madini, Sospeter Muhongo na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe.
Wizara ya Nishati na Madini pamoja na Shirika la Umeme (Tanesco), zimekumbwa na kashfa nyingine huku ikilezwa kwamba hali ya umeme nchini ni mbaya.
Hata hivyo, Meneja Mawasiliano wa Tanesco, Badra Masoud, amekanusha taarifa ya uwezekano wa nchi kuingia gizani, akieleza kwamba hali ya mabwawa sio mbaya.
Kashfa ya safari hii imeibuliwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mashirika ya Umma (POAC), Kabwe Zitto, kwenye mtandao wake wa Word Press.
Katika taarifa hiyo, Zitto alisema bwawa la Mtera hivi sasa lina kina cha maji chini ya kiwango kinachotakiwa na uzalishaji wa umeme ni asilimia 20 ya uwezo wake.
Alisema taarifa za kitaalamu zinaonyesha kwamba iwapo Tanesco wataendelea kutumia zaidi maji yaliyopo Mtera, mitambo itashindwa kazi na Gridi nzima ya Taifa itasimama maana Mtera ndiyo nguzo kuu ya Gridi ya Taifa.
“Hali hii ni hatari sana kwa uchumi na ulinzi na usalama wa Taifa. Kimsingi Gridi ya Taifa ipo hatarini kutokana na kiwango cha maji kilichopo Mtera hivi sasa na kuendelea kupungua kwa kina hicho cha maji,” alisema.
Hata hivyo, Meneja Mawasiliano wa Tanesco, Badra, alieleza: “Hali siyo mbaya na hatutegemei maji tu kuzalisha umeme. Tunatumia gesi na mafuta mazito.”
Wakati Tanesco ikiwa na msimamo huo, Zitto ameitaka wizara kuueleza umma nini kinachoendelea katika sekta ndogo ya umeme hapa nchini.
Alisema taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG), kuhusu zabuni za manunuzi ya mafuta ya kuendesha mitambo ya umeme wa dharura, iwekwe wazi kwa kuwa kuna ripoti kwamba wajanja wachache wamegeuza ununuzi wa mafuta ya kuendesha mitambo ya umeme kama mradi binafsi.
Alisema imebainika kwamba jumla ya Sh. bilioni 86 za kununua mafuta ya kuendesha mitambo ya umeme wa dharura kati ya Novemba, mwaka jana na Oktoba, mwaka huu, zimeibwa na maofisa waandamizi wa Wizara ya Nishati na Madini.
Hata hivyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakimu Maswi, hakukanusha wala kuthibitisha taarifa hizo badala yake alisema hana la kuzungumza.
“Mimi sijui chochote, siwezi kusema chochte leo (jana) kwa sababu sina taarifa hizo, niache nipumzike,” alisema Maswi.
Kuhusu hali ya umeme na hali ya Mtera, alisema “sijui chochote kwa sasa; sina cha kusema.”
Kwa upande wake, Zitto ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Fedha na Naibu Kiongozi wa Upinzani bungeni, alisema kutokana na mkanganyiko wa taarifa hizo, Wizara ya Nishati na Madini inapaswa kuueleza umma hali halisi ya sekta ya umeme nchini.
“Uzalishaji wa umeme upoje, hali ya maji katika bwawa mkakati la Mtera na nini hatma ya mitambo ya IPTL, kesi zake na utekelezaji wa mapendekezo ya Bunge kuwa kesi za kampuni hii zimalizwe nje ya mahakama. Pia Taifa lielezwe mpango wa dharura wa umeme unakwisha lini maana muda uliotolewa na Bunge Agosti, mwaka 2011 tayari umekamilika,” alisema.
Kadhalika, alimtaka Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, kueleza hatua alizochukua baada ya kukabidhiwa taarifa na CAG kuhusu maafisa waandamizi wa Wizara waliohusika na wizi wa Sh. bilioni 86 za kununua mafuta ya IPTL.
Hata hivyo, NIPASHE jana ilimtafuta Waziri Muhongo, lakini simu yake ya mkononi iliita bila kupokelewa.
“Waziri wa Fedha na Uchumi aueleze umma ni kiwango gani cha fedha Hazina imetoa kununua mafuta ya kuendesha mitambo ya umeme wa dharura kati ya Novemba mwaka 2011 na Oktoba, huu na kama taratibu zote za zabuni zilifuatwa na pale ambapo hazikufuatwa ni hatua gani PPRA (Mamlaka ya Ununuzi wa Umma), imechukua dhidi ya waliokiuka sheria ya manunuzi na kuleta hasara ya mabilioni ya fedha kwa Serikali,” alisema Zitto.
Alisema taarifa hiyo inaonyesha kuwa kuna kikundi ambacho kazi yake kubwa ni kujifaidisha binafsi na mpango wa umeme wa dharura kupitia manunuzi ya mafuta mazito ya IPTL.
Kashfa hiyo inakuja miezi kadhaa baada ya wizara hiyo kuandamwa na tuhuma za kutaka kuwahonga wabunge ili wapitishe bajeti yake Julai, mwaka huu.
Aidha, tangu mwaka 2011 kumekuwa na shinikizo lililotolewa na POAC, Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini na Waziri Kivuli wa Nishati na Madini kwamba zabuni za ununuzi wa mafuta ya kuendesha mpango wa umeme wa dharura na mchakato mzima wa manunuzi ya mafuta hayo ufanyiwe uchunguzi wa kina; jambo ambalo halijatekelezwa hadi sasa.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment