Waziri wa Fedha Dkt William Mgimwa akikata utepe wa uzinduzi wa maabara ya kisasa iliyogharimu milioni 49 ikiwa ni sehemu ya mradi wa vijiji vya Milenia wa Mbola jana wilayani Uyui wakati Waziri huyo alipotembelea Wilaya hiyo kuona mradi wa mfano ulivyoboresha maisha ya wananchi katika vijiji 16 zinavyoteleza mradi huo. Kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Uyui Said Shaban Ntahondi na kushoto ni Mbunge wa Jimbo Tabora Kaskazini Mamlo Shafin Sumar na wapili kutoka kushoto ni Kiongozi wa Mradi wa Vijiji vya Milenia wa Mbola Dkt Gerson Nyadzi.
Waziri wa Fedha Dkt William Mgimwa(kushoto) akiongea na viongozi wa vijiji 16 vinavyotekeleza mradi wa vijiji vya Milenia wa Mbola jana wilayani Uyui juu ya kuufanya mradi huo kuwa darasa endelevu kwa ajili ya vijiji vingine nchini kwenda kujifunza juu ya utekeleza wa malengo 8 ya Milenia . Waziri huyo alitembelea Wilaya hiyo kuona mradi wa mfano ulivyoboresha maisha ya wananchi katika vijiji 16 zinavyoteleza mradi huo. Katikati ni Mwnyekiti wa Halmashauri ya Uyui Said Shaban Ntahondi na kulia ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Ilolangulu Ally Magoha. PICHA na GCU – HAZINA
Na Mwandishi wetu -GCU-Hazina- Uyui- Tabora
Waziri wa Fedha Dkt William Mgimwa amewataka wakazi wa Wilaya ya Uyui mkoani Tabora waliopo katika wa utekelezaji malengo ya Milenia chini ya mradi wa vijiji vya Milenia wa Mbola kuufanya mradi huo kuwa endelevu kwa kutunza vizuri miradi yote iliyoibuliwa kwa ajili ya uboreshaji wa maisha ya wananchi wa eneo hilo .
Waziri huyo alitoa kauli hiyo jana wilayani Uyui mkoani Tabora mara baada ya kuzindua maabara iliyochini ya mradi huo ambayo imegharimiu shilingi milioni 49 hadi kukamilika.
Alisema kuwa ni vema wananchi hao wakahakikisha miradi yote iliyotekelezwa chini ya mradi wa vijiji vya milenia wa Mbola inatunza vizuri ili iwe darasa la kufundishi vijiji vingine hapa nchini katika utekelezaji wa malengo 8 ya milenia.
Dkt. Mgimwa aliongeza kuwa itasikitisha kuona kuwa mara baada ya muda wa mradi kuisha wa 2006-2012 na wafadhili ambao ni Milenia Promise Tanzania kumaliza muada wao na miradi inakufa na kusema kuwa hatua hiyo haitakuwa nzuri.
Aidha alitoa wito kwa wanavijiji wengine ambao hawapo katika mradi huo kwenda katika Kijiji cha Ilolanguru wilayani Uyui ili wajifunze jinsi ya utekelezaji wa malengo ya Milenia kwa kutumia juhudi za wananchi. Awali akitoa taarifa kwa Waziri wa fedha, Mwenyekiti wa Kijiji cha Ilolangulu Ally Magoha alisema kuwa katika utekelezaji malengo ya Milenia chini ya mradi wa vijiji vya Milenia wa Mbola wameweza kuboresha maisha yao katika vijiji 16 katika eneo hilo.
Alitaja manufaa waliyokwishapata ni pamoja na ujenzi wa nyumba za kisasa kwa kutumia matofali ya kuchoma na bati na kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula na fedha.
Mogoha aliongeza kuwa pia mradi huo umewawezesha kupunguza tatizo la vifo vya watoto waliopo chini ya maika 5 na mamawajawazito ambapo awali vifo vilikuwa wastani wa watoto watatu(3) hadi watano (5) na wanawake wajawazito 3 hadi 5 katika kipindi cha miezi mitatu lakini hivi sasa vifo ni wastani huo katika kipindi cha miezi sita na wakati mwingine hakuna.
Alisema kuwa hatua hii imefikiwa mara baada ya kuwaelimisha wananchi juu ya kutumia vyandarua na kuua mazalia ya mbu na hivyo kupunguza malaria katika eneo hilo.
vilevile Mwenyekiti huyo aliongeza kuwa kiwango cha wanafunzi wanaoishia njia(drop out) kimepungua mara baada ya mradi huu kuanza kwani mbinu mbalimbali zimesaidia watoto wengi kumaliza darasa la saba . Mbinu hizo ni pamoja na kutoa chakula kwa wanafunzi na kuhamasisha michezo mashuleni jambo liliwavutia watoto wengi.
kuhusu suala la maji alisema wanaendelea vizuri ambapo wastani wa asilimia 60 ya wakazi wa eneo hilo wanapata maji safi na salama. Mradi wa vijiji vya Milenia wa Mbola unatelelezwa katika vijiji vya Ilolanguru, Isenga, Ngokolo, Ulimakafu, Mpenge, Isila, Mbola, Kasisi A, Mabama, Ideka, Mbiti, Msiliembe, Iberi, Inonalwa, Usagari, Msima na Migungumalo.
No comments:
Post a Comment