Mimi ni nani mbelezako bwana mpaka ukanijalia kuwa hai hadi hii leo nakushukuru mungu kuniokoa katika majanga mbalimbali ya mwaka uliyopita hasa kwenye ile ajali iliyonitokea Mbalizi kwani zaidi ya watu 12 walifariki hayo ni baadhi ya maneno aliyokuwa akitamka Dr Mary Mwanjelwa kwenye ibada ya shukrani iliyofanyika katika kanisa la Moravian ushirika wa Ruanda jijini Mbeya
Dr Mary Mwanjelwa akiwa na naibu waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi Philipo Mulugo wakiimba kwa pamoja katika ibada hiyo ya shukrani
Ndugu jamaa na marafiki toka sehemu mbali mbali walihudhuria ibada hii ya shukrani
Tizo kijana aliyemwokoa mweshimiwa Dr Mary Mwanjelwa kwenye ajali mbaya iliyotokea mwaka jana maeneo ya mbalizi Mbeya hapa akielezea jinsi aliyomwokoa anasema ni mungu tu ndiye aliyetenda hayo maajabu kwani hakujua kabisa kama huyo dada ni mbunge wengi waliogopa kwenda kwenye gari alimokuwamo mbunge kwani moto mkubwa ulikua umeanza kuwaka akajikuta tu kaamua kwenda kwenye gari hiyo baada ya kuona mkono wa kuomba msaada na alipofika ilibidi avunje kioo cha gari hiyo na kumtoa Dr Mary Mwanjelwa kwenye gari hiyo huku moto ukiendelea kuwaka
Kijana Tizo akilia akisema huwenda mungu alikuwa na makusudi yake kunifanya mimi niwe daraja la kumuokoa dada Mary
Mchungaji Nyambo naibu waziri Mulugo na mkewe wakiwa makini kumsikiliza Tizo jinsi alivyomwokoa Dr Mary Mwanjelwa
Ndugu jamaa na marafiki wakimsikiliza Tizo
Hili ndilo gari alimokuwemo mweshimiwa mbunge Dr Mary Mwanjelwa katibu wake aliteketea kabisa kwenye gari hilo
dreva wagari ya mbunge kwa sasa anaendelea vizuri bado yupo kwenye matibabu DSM
Askofu wa Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini Magharibi Alinikisa Cheyo Ndiyo aliongoza ibada hiyo ya shukrani
Naibu waziri wa elimu Philipo Mulugo na Dr Mary Mwanjelwa wakicheza pamoja na kwaya ya Debora Mwaisabila kanisani hapo
Debora Mwaisabila akiwa na waheshimiwa wabunge wakimtukuza mungu kwa wimbo
Kwaya ya Paradise ikiimba kanisani hapo
Mweshimiwa mbunge Dr Mary Mwanjelwa ametoa msaada wa baiskeli 10 za walemavu wa miguu zenye dhamani ya shilingi milioni 2.5 hapa akiwa pamoja na walemavu hao baada ya kuwakabidhi baiskeli zao
picha na Mbeya yetu
No comments:
Post a Comment