Jaji Mkuu, Othuman Chande akikata utepe wakati wa uzinduzi wa Kitabu cha Sheria chenye maandiko ya kesi mbalimbali pamoja na jarida la makala, Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA), Jaji Engera Kileo na Msajili wa Mahakama Kuu Kitengo cha Biashara. (Picha na Prona Mumwi)
Mwendesha pikipiki akiwa amekiuka sheria ya usalama barabarani kwa abiria wake aliyemshika kuku kutovaa kofia ngumu (helmet), inayoweza kumkinga na madhara ya majeraha kichwani endapo ajali itatokea, kama walivyokutwa Kigogo Barabara ya Kawawa, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Abiria anapaswa kukataa kuhudumiwa na pikipiki kama hizi zinazokiuka sheria ili kuepuka madhara makubwa inapotokea ajali. (Picha na Charles Lucas)
Mkazi wa jiji akiwa na mzigo wa magodoro, kama alivyokutwa Barabara ya Nkrumah, Gerezani Dar es Salaam jana. Magodoro hayo ambayo ni mabaki kutoka viwandani hutumika kutengeneza mito ya kulalia na viti vya magari. (Picha na Charles Lucas)
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahimu Lipumba, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), Dar es Salaam jana, kuhusu mapendekezo ya chama hicho katika Katiba Mpya kuwapo kwa Serikali Tatu badala ya mbili za sasa. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Uchaguzi na Bunge, Bw. Shaweji Mketto. (Picha na Peter Mwenda)
Baadhi ya wapitanjia wakipita katika madimbwi ya maji yaliyotokana na mvua zinazoendelea kunyesha jijini, kama walivyokutwa Keko Machungwa, wilayani Temeke, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Eneo hilo limekumbwa na mafuriko na kusababisha baadhi ya familia kukosa makazi. (Picha na Charles Lucas)
Ofisa Mawasiliano wa Tanga Cement, Mtanga Noor (kulia) akisalimiana na baadhi ya wachezaji wa timu ya tenisi ya Tanzania katika hafla ya ufunguzi wa mashindano ya Kimataifa ya Tenisi ya Ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati kwa vijana yanayodhaminiwa na Tanga Cement kwenye Viwanja vya Gymkhana, Dar es Salaam jana.Na Mpigapicha Wetu
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa (kushoto), akikabidhi kiroba cha mchele kwa Meneja wa Kituo cha Kusaidia Watumiaji wa Dawa za Kulevya kuachana na matumizi hayo (Sober House), kilichopo Chakechake Pemba, Zanzibar Bw. Abdulwaheed Said (wa pili kulia), ni Meneja wa Vodacom Foundation Bi. Grace Lyon na Meneja Mahusiano ya Nje wa Vodacom Bw. Alum Mwalim hafla hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki (Picha nampigapicha wetu
(picha zote kwa hisani Majira)
No comments:
Post a Comment