ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, January 17, 2013

Kipa Nigeria kutembea mtupu

KIPA namba moja wa timu ya Taifa ya Nigeria ‘Super Eagles’, Vincent Enyeama amesema atavua nguo zote na kubaki na vazi la ndani tu na kuzunguka uwanja mzima iwapo kikosi chao kitatwaa Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka huu nchini Afrika Kusini.
Michuano hiyo ya 29, inaanza mwishoni mwa wikiendi hii, na filimbi ya mwisho ya mechi ya fainali itapulizwa Februari 10.

“Ni kama vile ndoto yangu itatimia kwa kutwaa ubingwa, nitafanya jambo rahisi lakini linaweza kuwa gumu kwa wengine. Nitavua nguo na kubaki na chupi kama furaha ya kutwaa taji,” alisema Enyeama.

Enyeama alikuwa na kikosi cha timu ya Taifa Nigeria kilichocheza michuano ya mwaka 2004, na 2010 kiliishia hatua ya nusu fainali.

Kabla ya hapo, mwaka 2008 Enyeama hakuwa chaguo namba moja la Kocha Austin Ejide na badala yake akafunikwa na Berti Vogts aliyepewa jukumu la kuwa namba moja.
Enyeama alirejesha makali yake baada ya kuondoka kwa Vogts na alitangazwa mchezaji bora wa fainali za Kombe la Dunia mwaka 2010 kwa timu ya Taifa Nigeria.

Nyota huyo anayecheza soka la kulipwa nchini Israel alisema: “Nia yangu ni kuendelea kucheza mpaka nikifikisha miaka 40 na kama itawezekana nifike hata miaka 42,” alisema Enyeama.
“Nafanya sana mazoezi, nataka kubaki kwenye kiwango changu kwa muda mrefu,” alisema zaidi. Kuhusu shinikizo kubwa linaloikabili Nigeria kutwaa taji tangu mara ya
mwisho mwaka 1994, alisema: “Kwa sasa naweza kusema sidhani kama ni sahihi kufikiria kutwaa taji. Kwanza lazima tushinde mchezo wa kwanza, wa pili na kusonga mbele zaidi.”
Mwananchi

No comments: