Kikosi cha Young Africans kilichoanza katika mchezo dhidi ya Black Leopard
Timu ya Young Africans Sports Club kesho alfajiri inatarajiwa kusafiri kuelekea jijini Mwanza ambapo siku ya jumatano itacheza mchezo wa kirafiki wa marudiano dhidi ya timu ya Black leopard kutoka nchini Afrika Kusini katika Uwanja wa CCM Kirumba.
Mchezo huo wa jumatano utakua ni fursa kwa wakazi, wapenzi wa soka wa kanda ya ziwa kuweza kuiona timu yao kwani tangu irejee nchini kutoka Uturuki imecheza mchezo mmoja tu wa kirafiki katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, hivyo ni fursa nzuri kwa wapenzi wa soka kanda ziwa kuiona timu yao.
Katika mchezo wa kwanza Young Africans iliibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Black leopard huku mabao ya Yanga yakifungwa na Jerson Tegete mabao mawili na Frank Domayo akifunga bao moja na pia kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa mechi hiyo.
Kocha Mkuu Ernest aliomba kupata michezo miwili ya kirafiki kabla ya kuanza kwa mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Vodacom ambayo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi mwishoni mwa wikii hii katika viwanja tofauti, Yanga ikianza na timu ya Prisons siku ya jumapili.
Aidha Black Leopard ambayo iko nchini Tanzania kwa ajili ya maandalizi ya mzunguko wa pili wa ligi kuu nchini Afrika kusini PSL imesifia mchezo wa juzi dhidi ya Yanga na kusema ulikuwa mchezo mzuri na wakuvutia japokuwa walifungwa, lakini watajitahid kupata ushindi katika mchezo wao wa marudiano siku ya jumamosi.
Young Africans ambayo itatumia mchezo huo kama maandalizi yake ya mwisho, itaondoka kesho alfajiri na msafara wa watu 37, wachezaji 27, benchi la ufundi 7 na viongozi 3.
Timu itarejea Dar es salaam siku ya alhamis jion tayari kabisa kwa kujiandaa na mchezo wa kwanza wa mzunguko wa pili wa ligi Kuu ya Vodacpm dhidi ya timu ya Prisons ya Mbeya.
Kuhusu viingilo vya mchezo huo ni vitakua ni Jukwaa Kuu Tshs 10,000/=, na mzunguko Tshs 3,500/=
No comments:
Post a Comment