Jeshi la polisi Arusha limelazimika kutumia mabomu ya machozi kutawanya wanafunzi.
Jeshi la polisi mkoa wa Arusha limelazimika kutumia nguvu na mabomu ya machozi kuwatawanya maelfu ya wanafunzi wa chuo cha uhasibu Arusha kwa kufanya vurugu na kuwakamata baadhi ya wanafunzi pamoja na wakili maarufu Albert Msando huku mbunge wa Arusha Goodbless Lema anatafutwa kwa tuhuma za kuwachochea wanafunzi hao kufanya fujo.
1 comment:
Hicho ni kimoja kati ya vigezo vinavyopima ubora wa elimu duniani. Unapotoka nje ya nchi ukajitambulisha kuwa ulipata degree Tanzania, unaonekana umechanganyikiwa. wenzentu wanaamini kuwa kama elimu ingekuwa ni binadamu, basi degree za Tanzania zipo matakoni. Zinatoa wasomi wanaojenga maghorofa yanayodondoka kwa kupulizwa na upepo na kuruhusu watu kutumia maboti Dar baada ya mvua ya dakika tano. Hii ni kwa sababu msomi wa kiTanzania lazima aandamane, apigwe mabomu, mikopo ichelewe,aibiwe,abakwe, alawitiwe, auawe, akamatwe na polisi, na chuo kifungwe na kufunguliwa kwa wakati anaotaka waziri eti kwa sababu watoto walimshangilia mbunge wao na kumzomea mkuu wa mkoa. Yote hayo nanafanyika ndani ya muda uliopangwa wa kupata degree bila kufidia muda uliopotea.
Post a Comment