ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, April 24, 2013

WAUMINI KKKT MORO WAPINGANA UNUNUZI WA SAA YA MCHUNGAJI

Mchungaji Gyunda akitoa saa yake ipigwe mnada kuchangia ujenzi wa kanisa
Mwinyirisiti Ndosi[kushoto] akipokea saa hiyo kutoka kwa mchungaji…
Mchungaji Gyunda akitoa saa yake ipigwe mnada kuchangia ujenzi wa kanisa
Mwinyirisiti Ndosi[kushoto] akipokea saa hiyo kutoka kwa mchungaji Gyunda
Mwinjiristi Ndosi akimkabidhi Mlyapatali aipige mnada saa hiyo
Saa hiyo ikipigwa Mnada huku baadhi ya ya waumini wakishuhudia kwa huzuni tukio hilo
Waumni hao wakiendela na Mchango kupinga muumini wenzao kuinunua saa hiyo
Wazee wa kanisan hilo wakihesabu fedha zilizochnga kwa lengo la kuikomboa saa ya Mchungaji huyo
Mwinjiristi Ndosi akimludishia saa yake mchungaji huyo kwa sytali ya kumvisha huku akitabasamu
Mchungaji Mary aliyenzisha mchakato wa kuchangisha fedha za kuikomboa saa ya mchungaji Gyunda akimpa mkoni wa ponge chungaji Gyunda kwa moyo wake wa kijitolea
Mzee Mushi ambaye ni mzee wa kanisa hilo akimpa mkono wa asante mchungaji Gyunda kwa kutoa saa yake sadaka
Mchungaji Guyunda akimtambulisha rafiki yake Bw Eliewaha Mshna kulia] ambaye ndiye aliyesababisha kuja mkoani Morogoro
Mchungaji Gyunda akiondoka madhbahuni huku akiwapungia waumini hao waliokuwa wakimshjangilia kwa nguvu
Baada ya ibada hiyo baadhi ya waumini walimfuatia mchungaji huo na kumpongeza
Hili ndio kanisa ni KKKT usharika wa Mji Mpya ambalo kwa sasa linaendela kujengwa kwa nguvu wa waumini wa kanisa hilo.

KATIKA hali isiyo ya kawaida waumini wa Kanisa la Kiinjiri Kirutheri Tanzania’KKKT’ dayosisi ya Morogoro usharika wa Mji mpya wamempinga vikali muumini mwenzao aliyeonyesha nia ya kununua saa ya Mchungaji aliyeitoa sada ya uchangiaji wa ujenzi wa kanisa lao.

Tukio hilo lilichukua nafasi jumapili iliyopita kwenye ibada ya kwanza iliyofanyika ndani ya usharika huo unaokadilikuwa kuwa na waumini wengi kuliko sharika nyingine kwenye dayosisi hiyo.
Aliyesababisha hali hiyo ni mchungaji mgeni aliyejitambulisha kwa jina la Edward Gyunda ambaye ni mwanafunzi wa chuo kikuu cha St Jonh’s kilichopo mkoani Dodoma

Mwinjiristi Ndossi aliyekuwa akiongoza ibada hiyo baada ya kumuona mchungaji huyo aliyekuwa amevaa kora ya kichungaji shingo alimuarika madhebahuni kwa lengo la kuwasalimia waumini hao na kwamba baada ya salamu mchungaji huo aliomba mmoja wa waumni hao afungue biblia na kusoma Eziroi 10 mstari wa 4- 8 
“ Mameno hayo yana lengo la kuwatia nguvu katika kazi hii ya kumjengea mungu nyumba ya ibada,mimi ni mwanafunzi nachukua Masters of Arts in Communty Doverppment pale chuo kikuu cha St John Dodoma,hapa sina pesa yoyote mfukoni lakini nitatoa saa yangu niliyopewa zawadi mwaka 2007 kule Marekani ipigwe mnada kwenye ibada hii na pesa zitakazopatikana ziwe sadaka yangu kwenye ujenzi wa kanisa lenu”alisema mchungaji huyo ambaye kabla ya kujiunga na chuo hicho alikuwa akiongoza usharika wa Ndago KKKT dayosisi ya Kati mkoa wa Singida, 

Baada ya kusema maneneo hayo alivua saa hiyo na kumkabidhi mwinjiristi ambaye naye alimkabidhi muumini Mwalupanga Mlyapatali ambaye ni mwanakwaya wa kwaya ya Sifuni aipige mnada,
Muumni mmoja ambaye hakuwa tayari kutaja jina lake alitoa ofa ya kuinunua saa hiyo kwa shilingi elfu 50,baada ya kutolewa kwa Ofa hiyo mchungaji mwingine mgeni Bi,Mary Nnko kutoka usharika wa Kihonda ambaye alialikwa kutoa huduma kwenye ibada hiyo kufuatia mchungaji kiongozi wa usharika huo Thomas Poul kwenda likizo alisimama na kutoa shilingi elfu 10 akiomba asapotiwe ilifike elfu 60 za kumpiku muumni huyo nakuomba saa hiyo arejeshewe mwenyewe.
Waumini hao waliti ombi hilo na kuchanga kiasi cha shilingi laki moja, kufuatia hali hiyo muumini huyo aliamu kupanda dau na kuwapiku wenzake na kudai kwamba saa hiyo asiludishiwe mchungaji angeinunua kwa shilingi laki moja na elfu 25.

Wakati mnadishaji huyo akihesa kwa lengo la kumkabidhi saa hiyo kwa mara nyingine tena waumini hao waliungana na kuchanga tena na kufanikiwa kufikisha laki 276,700 na kwamba muumini huyo kingang’anizi alichemka hivyo saa hiyo alirudishiwa mwenyewe ambapo wakati anakabidhiwa kanisa zima lilipuka kwa shangwe na vigerege huku baadhi yao wakimtazama muumini huyo kwa jicho la kejeri. 

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Mchungaji Gyunda alidai kwamba ljumaa iliyopita alifika mkoani hapa kumtembelea rafiki yake Bw Eliewaha Mshana akitokea Dodoma” Leo nimeamu kuja kusari hapa nilipofika niliguswa na habari za ujenzi wa kanisa hili na sikuwa na pesa hivyo nilisukumwa na roho mtakatifu kutoa saa yangu niliyopewa zawadi nilipotembelea marekani mwaka 2007. na huyo rafiki yangu alidai kwamba saa hii alinunua dolla 60 namshukuru mungu saa imeludi na nimeweza kuchngia ujenzi wa kanisa hili kwa shilingi laki tatu kasoro kidogo” alisema chungaji huyo.

Kwa Upande wake muweka hazina mkuu wa usharika huo Bw Judika Uroki alipotakiwa kuzungumza tukio hilo alimsifu mchungaji huyo na kudai kwamba hilo pia ni fundisho kubwa kwa waumni wote ulimwengunmi kwamba sadaka sio lazima pesa kitu tuchoche ni sadaka kwa Mungu. Baada ya ibada hiyo kukamilika waumini wengi hasa wanaotoka mkoa wa Singida walimzingira Mchungaji huo kila mmoja akitafuta nafasi ya kumpongeza kwa kushikana naye mkono.
HBR: PICHA NA DUSTAN SHEKIDELE,Morogoro.
GPL



No comments: