ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, April 18, 2013

'Dawa za kuongeza nguvu za kiume sasa tishio Z'bar'

Waziri wa Afya Zanzibar, Juma Duni Haji.
Waziri wa Afya Zanzibar, Juma Duni Haji, ameshangazwa na wimbi la uuzaji wa dawa za nguvu za kiume uliojitokeza katika maeneo ya misikiti visiwani humu.
Akifunga mjadala kuhusu ripoti ya Kamati ya Maendelo na Ustawi wa Jamii, Wanawake na Watoto ya mwaka 2012/2013 , Duni alisema waganga wamevamia maeneo ya misikiti na kuuza dawa za kienyeji zinazodaiwa kuongeza nguvu za kiume.
Duni alisema inashangaza kuna dawa zinazouzwa na za wanaume pekee lakini akasema ni jukumu la wananchi wenyewe kuwa makini kwa vile siyo kila daktari wa tiba asilia anaweza kutibu kila aina ya maradhi.
Hata hivyo, alisema kwa upande mwingine, vyombo vya habari vimekuwa vikichangia kuwaingiza wananchi katika matumizi ya dawa ambazo hazijathibitishwa ubora wake kutokana na kutangaza bila kupata ukweli wa dawa hizo.
Alisema baadhi ya dawa zinazouzwa huchangia matatizo ya wagonjwa kutokana na kuzitumia bila  maelekezo ya kitaalam, hivyo wanapozidiwa na kwenda hospitali, ugonjwa huwa mkubwa na wengine kupoteza maisha.
Hata hivyo, Duni alisema ataendelea kusimamia ukweli kwa vile umri wake unafikia ukingoni.
Alisema serikali imeshatunga Sheria ya Afya ya Jamii na Mazingira namba 11 ya mwaka 2012 ambayo itasaidia kuondoa matatizo ya matumizi mabaya ya tiba asilia.
CHANZO: NIPASHE

3 comments:

Aliweiwei Machibya said...

Inashangaza sana Waziri huyu kuingilia uhuru wa mtu binafisi inamhusu mhusika mwenyewe, ana hiari ya kutumia ama kutotumia hii siyo dawa ya kulevya bali ni kichocheo cha nguvu za kiume kina madhara au la ni uamuzi wa mtumiaji, Sioni haja Serikali kuingilia kati bali ifafanunue faida na hasara za utumiaji wa madawa haya, Mapenzi ni mhimu katika ndoa , kitandani ni mwisho wake.

Anonymous said...

NAIONAJE HII STORY IMEKAAJE SI YA KISHARI SHARI NA TENA ETI INASEMA HIZI DAWA ZINAUZWA MISIKITINI CAN YOU IMAGINE THIS, TUMESOMEA TAALUMA YA UANDISHI WA HABARI NA PSYCHOLOGIA NA TUNAJUA MTU ANAPOA ANDIKA AU KUTUMA KITU ANAKUSUDIA NINI LAKINI KWA MWANANCHI WA KAWAIDA ATAONA POA HII STORY ACHENI BWANA ZENU HIZO WATU TUMESHAFUNGUKA SIKU HIZI MACHOO MEUPE HATA USIKU TUNAONA JUWA KALIIII

Anonymous said...

kazi kweli kweli haya tena wawa nyuke wana wariii wasike adabu zaoo ha ha ha