Timu ya Veteran ya DMV itacheza mechi na vijana wa DMV leo alhamisi July 4, 2013 kwenye uwanja wa Heurich Turf Field Address 6601 Ager Road, Hyattsville, MD 20782 uliochezewa Yanga na Simba, Mpambano huu umekua gumzo kubwa hapa DMV kwa timu ya vijana wakielekea kuogopa kucheza na Veteran kwa visingizio vya hapa na pale. Mechi iiraanza 7:pm sharp
Masanja Mkandamizaji ndiye atakaeongoza benchi la Vijana . Wasanii hao ambao wapo nchini maalum kwa tamasha la utamaduni wa kiswahili Marekani na sherehe ya miaka 3 ya Vijimambo ambalo litafanyika siku ya Jumamosi July 6, 2013, Capitol Heights, Maryland na Mhe. Rais Mustaafu Ali Hassan Mwinyi ndiye atakayekua mgeni rasmi.
Timu ya Vijana ambao haijataja kikosi cha timu yake huku kukihofiwa huenda wakachomoa kwa kutoleta timu uwanjani. Veteran wao wanasema kazi ni moja tu kama tik tak, tik tak weka kati Vijana wataokota sana mpira wavuni.
1 comment:
wageni rasmi wameishaaaaa? mpaka shilole!na lazima kuna jambo na wewe kwa wanawake wa summer!
Post a Comment