Boti Mpya ya Kilimanjaro 4 ikiwa katika bandari ya forodhani baada ya kushusha katika meli ilioileta Zanzibar.
Sehemu ya Daraja la Kwanza katika Boti mpya ya Kilimanjaro 4.ikionekana katika picha baada ya kufunga gati katika bandari ya malindi leo.
Meneja Mkuu wa Azam Marine Hussein Mohammed Said, akizungumza na waandishi wa habari akiwa katika boti hiyo wakati wa majaribio yaliofanyika leo baada ya kuwasili, boti hiyo ina uwezo wa kuchukua abiria 700 kwa wakati mmoja na mwendo wa dakika 70 hadi Dar.
Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vilioko Zaanzibar wakishuka katika boti ya Kilimanjaro 4 baada kurudi katika majaribio ya boti hiyo yaliofanyika baada ya kushushwa leoZenj....
Mkurugenzi Mkuu Kampuni ya Azam Marine Said Bakresa, akiwa na Ofisa wa Kampuni yake Abrazak wakati wa majaribio ya Boti hiyo ilipowasili katika bandari ya Zanzibar.
Meneja Mkuu wa Kampuni ya Azam Marine Hussein Mohammed Said, akizungumza na mwandishi wa habari Abdalla Majura, kuhusiana na ujio wa boti ya Kilimanjaro 4,
Wananchi wa Visiwani Zanzibar wakiangali ushushwaji wa Boti Mpya ya Kampuni ya Usafiri wa baharini ya Azam Marine
No comments:
Post a Comment