Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage akipeana mikono na Mkurugenzi wa Azam Media, Abubakar Bakhresa kulia baada ya kuingia Mkataba huo.
Kampuni ya vyakula ya Azam ya Dar es Salaam imenunua haki za televisheni za kipindi cha Simba kujitangaza kibiashara kwa miaka mitatu kwa malipo ya jumla ya sh. milioni 331, ilielezwa juzi.
Na katika kutekeleza makubaliano hayo uongozi wa kampuni tanzu ya Azam Media juzi uliikabidhi Simba, ambayo leo itakuwa na mkutano unaopingwa na baadhi ya wanachama, hundi 10 za jumla ya sh. milioni 100.
Hata hivyo, Azam Media ilikataa kueleza katika hafla hiyo kama inamiliki kituo cha televisheni licha ya kueleza kuwa kipindi hicho cha Simba kitaonekana kupitia ving'amuzi vya kampuni hiyo hivi karibuni.
Baada ya hafla hiyo ya utiaji sahihi wa makubaliano na malipo ya awali, ilielezwa kuwa awamu ya pili ya malipo ya sh. milioni 110 itakuwa mwakani na kiasi cha sh. milioni 121 kitalipwa mwaka 2015.
Kutokana na udhamini huo, Azam Media itakuwa ikirusha kipindi cha 'Simba TV Show' kuanzia hivi karibuni hapa nchini, ilielezwa.
Akikabidhi hundi hizo, Meneja Mkuu wa Azam Media, Said Mohammed alisema wameamua kuidhamini klabu hiyo ili kusaidia maendeleo ya "timu yao ambayo ni kongwe hapa nchini."
Mohamed alisema kupitia kipindi hicho wanachama na wapenzi wa Simba watafahamu klabu yao inavyoendeshwa na namna ya kuichangia ili kuharakisha maendeleo ya timu hiyo.
Baadhi ya wanachama wa Simba kwa muda mrefu wamekuwa hawaridhishwi na jinsi klabu yao inavyoendeshwa na uongozi wa mwenyekiti Isamil Rage.
Wanachama hao wanapinga mkutano mkuu wa wanachama huo uliotishwa leo kwa madai kuwa taarifa ya siku 14 ya kikao hicho inavunja katiba ambayo inataka wanachama wataarifiwe siku 30 kabla.
"Ili timu ya soka iwe na mafanikio ni lazima kuwe na vitu muhimu vitatu ambavyo ni uongozi bora, ari na nia na vile vile mpira wa sasa ni fedha na leo ndiyo maana tumefikia hatua hii," alisema Mohammed.
"Tunaleta mapinduzi katika soka la Tanzania".
Alisema kila kipindi kitakachorushwa kitakuwa kimetengenezwa na klabu ya Simba na Azam kama wadhamini watakirusha hewani kikiwa na matangazo ya bidhaa za kampuni hiyo.
Mbali na kumiliki Azam Media, kampuni ya Azam ambayo inajishughulisha zaidi na uuzaji na usambazaji wa nafaka miongoni mwa vyakula kadhaa, inamiliki washindani wa Simba kwenye ligi kuu ya Bara, klabu ya Azam.
Katika hafla ya kusaini mkataba huo, mmoja wa wadhamini wa Simba, Hamisi Kilomoni alieleza imani yake kuwa klabu hiyo itapiga hatua na kwamba kwa makubaliano hayo tayari Simba na Azam zimeongeza mahusiano.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment