Picha
ya mzee lifiga
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania inasikitika kutangaza kifo
cha aliyekuwa mtabiri bingwa wa kwanza wa hali ya hewa na
mkurugenzi mkuu wa kwanza wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania Bw. Urban Blass
Lifiga. Bwana Lifiga alizaliwa tarehe 27
Novemba 1936, kifo chake kilichotokea Jumatatu tarehe 15 Julai 2013 mchana katika
hospitali ya Bosph Mbezi kwa Msuguli Dar es Salaam.
Bwana Lifiga alikuwa mtabiri bingwa wa kwanza Tanzania na Mwaafrika
wa kwanza kujiunga Idara ya Hali ya Hewa ya Afrika Mashariki iliyokuwa chini ya
Jumuia ya Afrika Mashariki, ambayo kwa wakati huu makao yake makuu yalikuwa
Nairobi, Kenya. Bwana Lifaga aliteuli kuwa Mkurugenzi Mkuu wa kwanza wa
iliyokuwa Idara Kuu ya Hali ya Hewa, Tanzania. Alishisiriki na kushauri
Serikali katika kuanzisha kwa Idara hiyo.
Pamoja na nafasi ya Mkurugenzi Mkuu pia alichaguliwa kuwa
Mjumbe wa kudumu wa Tanzania katika Kamati Kuu ya Shirika la Hali ya Hewa
Dunia. Nafasi nyingine aliyeishika wakati wa uhai wake ni Kaimu Mkurugenzi wa
Idara ya Hali ya Hewa ya Afrika Mashiriki.
Bwana Lifiga atakubumbuka kwa mchango wake mkubwa katika
kuendeleza sayansi ya hali ya hewa nchini, Afrika na Duniani.
Ni mmoja kati ya wanasayansi waliokuwa zao la chuo kikuu cha
Makerere na alichukua shahada ya udhamili chuo kikuu cha Nairobi. Hapa nchini
alipata mafuzo ya Sekondari katika shule za Kwiro Sekondari, Mahenge na Pugu
Sekondari, Dar es salaam.
Mazishi yanatarajiwa kufanyika Ijumaa tarehe 19 Julai 2013 nyumbani kwake Msakuzi.
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania inajumuika na familia,
ndugu, jamaa na marafiki katika kuomboleza msiba huu.
Bwana ametoa, bwana ametwaa, Jina lake lihimidiwe; AMENI
IMETOLEWA NA OFISI YA
UHISIANO MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA
No comments:
Post a Comment