ANGALIA LIVE NEWS

Friday, July 5, 2013

MWANAMUZIKI LINAH BADO HAJUI JINA LA ALBUM YAKE

MWANADADA kutoka katika Nyumba ya Kukuza Vipaji Tanzania (THT), Linah Sanga ‘Linah’, amesema yuko katika hatua za mwisho kukamilisha albamu ambayo itakuwa na nyimbo nane, lakini tatizo kubwa linalomuumiza kichwa ni jina la albamu hiyo.
Akizungumza na Jambo Leo Dar es Salaam jana, Linah, alisema albamu hiyo itakuwa na nyimbo nane, lakini hadi sasa bado hajaipa jina kwani hajui ni nyimbo gani ambazo zitakuwepo ndani ya albamu hiyo kutokana na ubora wa nyimbo zake zote alizokuwanazo
inah alisema hadi sasa hajajua ni wimbo gani unaweza kuwa mzuri kwa ajili ya kuvutia albamu yake kwani anahitaji kufikiria ndipo baadaye aweze kupata jina litakalofaa
“Siwezi kusema kwamba albamu yangu imekamilika, hivyo kwa sasa nipo katika maandalizi ya kukamilisha na kama unavyojua katika kazi lazima uwe na mipango, hivyo najaribu kuangalia baadhi ya nyimbo zangu ambazo naamini zitauza albamu ili niziweke,” alisema.
Linnah aliwaomba mashabiki kukaa mkao wa kula kwa ajili ya kuipokea albamu hiyo, ambayo bado hajajua aipe jina gani ambalo litaweza kuiuza

No comments: