Na Mwandishi WetuCHOKOCHOKO zinazoendelezwa na Rais wa Rwanda, Paul Kagame dhidi ya Rais Jakaya Kikwete zimewakasirisha baadhi ya wananchi wakiwemo askari wa Tanzania na wakadai kuwa kiongozi huyo wa Rwanda atakiona cha moto akianza uchokozi.
Wakizungumza na gazeti hili mwishoni mwa wiki iliyopita kwa sharti la kutoandikwa majina yao gazetini, baadhi ya askari walisema wanamshangaa Kagame kuitishia Tanzania wakati anajua kuwa hana ubavu wa kupigana nayo.
Askari wengi waliohojiwa, walisema Rwanda haina uzoefu wowote katika vita ya kimataifa ukilinganisha na Tanzania na Kagame akianzisha vita ni yeye atakayekufa kwa sababu vita haina macho.
“Kagame anajua kwamba Rais Kikwete si mgomvi na alimpa ushauri tu kwa kumwambia azungumze na waasi nchini mwake sasa kwa nini anaendelea kufanya chokochoko? Akianza vita itamuua. Kwa nini anamdhalilisha rais wetu?” alisema askari mmoja.
Akaongeza: “Kagame amezoea vita ya wao kwa wao lakini Tanzania tumeshakwenda nchini Comoro ili kumng’oa Kanali Mohamed Bacar ambaye alikuwa aking’ang’ania madaraka katika Kisiwa cha Anjouan, tulipigana na Nduli Iddi Amin na akakimbia nchi, sembuse Kagame?” alihoji askari huyo.
Akaongeza: “Tumekwenda Msumbiji, Angola, Visiwa vya Shelisheli, Darfur na hata Lebanon, siyo kwa kuvamia bali kwa kuombwa na mataifa, hivyo Kagame aache kabisa kumkashifu rais wetu, amheshimu kama anavyoheshimiwa yeye.”
Licha ya askari, wananchi mbalimbali waliohojiwa na gazeti hili, wamemshangaa Kagame kwa kumtusi Kikwete.
“Kwangu mimi nasema ni bora tukaachana na huu mpango wa Shirikisho la Afrika Mashariki kwa sababu dalili mbaya zinaonekana hata kabla ya kuungana,” alisema Naomi Erasto, Mkazi wa Masaki, Dar.
Akaongeza kuwa Kagame ni lazima atambue kwamba Watanzania wapo tayari kuilinda nchi yao kwa gharama yoyote na kamwe hawawezi kuwa vibaraka wa Rwanda.
Rais Kikwete alimpa ushauri Kagame wakati wa mkutano wa kujadili amani na mpango wa ulinzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo uliofanyika katika Makao Makuu ya AU, Addis Ababa, Ethiopia mwaka huu.
Katika ushauri huo, Rais Kikwete alisema kwamba ni vyema Rais Kagame akakaa katika meza ya mazungumzo ya amani na Rais wa Kongo, Joseph Kabila ili kumaliza tofauti zao badala ya kutumia nguvu za kijeshi.
Badala yake, Kagame akajibu: “Nimekaa kimya kwa kipindi kirefu na kwa jinsi nilivyoweza kwa sababu nilifikiri kwamba mazungumzo ya kipuuzi yaliyozungumzwa na watu wajinga yamemalizika,” alisema Rais Kagame.
Akasema ushauri huo wa Rais Kikwete ni sawa na kuwachezea Wanyarandwa mbele ya mataifa.
Kagame aliyasema hayo katika sherehe za kuhitimu mafunzo ya maofisa wa jeshi wapatao 45 katika kituo cha mafunzo huko kwao na alipowahutubia vijana, Juni 30, 2013 kwenye mkutano wao wa “Youth Konnect” uliofadhiliwa na mke wake, Janet Kagame.
Kwa mara ya kwanza, Rais Kikwete alimtolea uvivu Rais Kagame mwishoni mwa wiki iliyopita, akasema ushauri ule aliutoa kwa nia njema kabisa kwani bado anaamini kuwa kama jambo linaweza kumalizwa kwa njia ya mazungumzo, ni vyema itumike.
“Isitoshe, ushauri ule niliutoa pia kwa Serikali za Kongo na Uganda. Katika mkutano ule Rais Museveni wa Uganda aliunga mkono kauli yangu. Rais Kagame hakusema chochote pale mkutanoni.
“Kwa upande wangu sijasema lolote kuhusu Rwanda pamoja na maneno mengi ya matusi na kejeli yanayotoka kwenye vinywa vya viongozi wake dhidi yangu. Siyo kwamba siambiwi yanayosemwa au sijui kusema au sina la kusema, la hasha, sijafanya hivyo kwa sababu sioni faida yake,” alisema Kikwete.Chanzo Global Publisher blog
7 comments:
Watanzania acheni kuchochea mambo kwa maneno kama mazoea yenu watru wanawaza maendeleo ninyi mnawa fitina na migongano ebu muerevuke basi this so crazy.
ndio waruwanda tumezoea vita na hatotuweza mnafikiri sisi tunabebwe kama mlivyo bwebwe nyinyi, eti nduli mmemtoa propaganda za kivita hatuwezi jaribuni kwanza nduli mlisaidiwa na mataifa ya nje other wise msingeweza hata kidogo kumgoa iddi amin dada the great na pia huko commorro mmesaidiwa mnazani sisi tumelala siyo jaribuni mtajuta si mchezo ruandwa ya leo si ya jana jaribuni tu
TANZANIA HAMNA UBAVU WA KUWAPIGA WARANDWA JARIBUNI BASI MTAKIONA KILICHO MTOA KANGA MANYOYA YAKE AU KWA NINI KUKU HANA MAZIWA YAKUKAMULIWA
Nyie Wanyarwanda acheni kujidanganya nyie. Nani haijui Rwanda? haina jenshi ispokuwa inamamluki. Kama ni kubebwa nyie ndiyo mliobebwa mlipomuua Habyarimana.
Swali dogo tu, YOTE HAYA KWA FAIDA YA NANI???
Nyie acheni ugomvi. Afrika yote ni moja.Mnatazamwa, wauza silaha wanatafuta soko. Wakuu watapigana mda wao ukiisha. Msihukumu wengine wasio na hatia.Watoto,wazee,vilema,na wengine mtawaharibia future. Resolve your conflicts diplomatically.Investments zetu zitasimama.
Kagame is a sick man(reminiscent of Iddi Amin Dada). He should just shut-up and spare his people from catastrophe. Rwanda as a land-locked country, needs Tanzania more than the other way round. It has depended on Tanzania for so many years. Many Rwandese have been given refuge and citizenship in Tanzania. History is in our favor. Unfortunately, stubborn tutsis and their deranged leader Kagame, poses the greatest threat to peace in the great lakes region. However, Kagame's days are numbered, and personally, I see no imminent threat from Rwanda which can shake Tanzania's resolve. We have East Africa's best trained, most experienced, and the mightiest fighting Army. Can Rwanda wake up the sleeping lion and escape the onslaught? We have helped and liberated many African countries (Zimbabwe, Namibia, Angola and Mozambique, bears witness). I feel sorry to the people of Rwanda! Tanzania forces can take over Kigali in less than seven days, giving enough time for Kagame to flee to Brussels or Paris.
Post a Comment