ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, August 6, 2013

Ulimis? Kwa nini Mbunge wa Nzega Hamis Kigwangalla hatompa kura Lowassa 2015

Mbunge wa Nzega Hamis Kigwangalla amesema hawezi kumpa kura yake Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli Mheshimiwa Edward Lowassa endapo jina lake litajitokeza kama mmoja ya wagombea urais, ni kauli ya Kigwangalla akijibu swali aliloulizwa na Mtangazaji Fina Mango katika kipindi cha Makutano kuhusu vuguvugu la urais 2015 linaloendelea ndani ya CCM juu ya mgombea urais ambapo Edward Lowassa ni kati ya wanaotajwa sana kama wagombea hasa katika mitandao ya kijamii.

“Sitompa kura Mheshimiwa Edward Lowassa kwa sababu za msingi tu, kwamba ninakipenda chama changu na nina hakika chama changu kikija na mgombea kwenye uchaguzi mkuu 2015 ambaye ana historia ya kuhusishwa na mambo machafu kama yale ya Richmond, Dowans ambayo unayasema, hapa tunaweza kupata tabu sana kuomba kura kwa wananchi, lakini pia tutakuwa tumewapa hoja wapinzani wetu ya kusema tunalea ufisadi, tunaubembeleza ufisadi kwa mikono miwili’ Kigwangalla

Kwenye sentensi nyingine Kigwangalla amesema Tanzania aihitaji rais asiyeweza kusimamia ukweli ambapo kuhusu ishu ya dowans amesema haoni tatizo la mitambo hiyo isipokuwa uamuzi uliotumika katika upatikanaji wake.

Kwenye hii interview, Kigwangalla alitangaza nia ya kugombea urais mwaka 2025 na kusema 2015 anaona bado ni mapema kwake kwani anaamini watanzania bado hawajamjua Hamis Kigwangalla ni mtu wa aina gani.

5 comments:

Anonymous said...

Mr Kigwangala uko sawa kabisa na tuko wengi wenye msimamo kama wa kwako. Tutaenxelsa kumpa heshima kijana wetu wa siku nyingi Mr Lowassa endapo ataweka swala hilo pembrni achilia mbali mambo anayofanyia wananchi kupitia vyanzo vya aina mbalimbali. Pole watanzania tujielimishe kuelekea 2015!.

Anonymous said...

The "word".

Anonymous said...

Good on you MP, the CCM machinery will have the last say. The guy I am told controls 80% of the possible members to the Congress, so he will get through but I hope the people had not forgoten on what happened.

Anonymous said...

Watanania wapo gizani hadi leo na bado hawajamsahau aliyewaweka gizani. Muache samaki ajikaange kwa mafuta yake.

Anonymous said...

Nakupongeza mbunge Kingwangala na msimamo wako wa kumpinga Lowassa. Tupo wengi ughaibuni tunaompinga Lowassa, na tutakusanya fedha za kutosha kuweza kuendesha kampeni ya kumpinga kuanzia vijijini, kata, tarafa, wilaya na mikoa yote nchini. Tunaomba wabunge wengine pale Dodoma wajiunge nasi kwani hatuwezi kumchagua kiongozi ambaye yupo tainted na scandals. Tunao viongozi wengi clean ambao wanaweza kugombea urais, siyo bwana Lowassa. Tutahakikisha tunakampeni dhidi ya wabunge wote wanaomuunga mkono Lowassa nao wasirudishwe tena bungeni.