Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Padre Joseph Mwang'amba alipokuwa akitoa maelezo jinsi alivyopata mkasa wa kumwagiwa tindikali jana.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Padre wa Kanisa la Romani Katoliki Parokia ya Machui, Joseph Mwang'amba, alipofika katika Hospitali ya Mnazi Mmoja kumpa pole, Mjini Unguja, baada ya kumwagiwa tindikali Mjini Magharibi - Zanzibar.
Mmoja wa Ndugu wa Padre aliyemwagiwa tindikali akimueleza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, hisia zake kwa uchungu kutokana na kitendo hicho cha kumwagiwa tindikali Padre na kuomba hatua zilichukuliwe ili kukomesha vitendo kama hivi ambavyo vimeanza kuzoeleka.
Hali ya usalama kwa watu visiwani inazidi kutetereka, huku viongozi wa Kanisa Katoliki, wakizidi kushambuliwa.
Safari hii, Padre Joseph Mwang’amba wa Parokia ya Machui mjini hapa, amemwagiwa maji yanayoaminika kuwa tindikali.
Padre Mwang’amba, alishambuliwa na watu wasiojulikana jana saa 10:00 jioni, akiwa anatoka kwenye mgahawa wa ‘intaneti’ wa Sun Shine uliopo Mlandege.
Waliommwagia tindikali hiyo walitoweka na Padri Mwang’amba kurudi ndani ya mgahawa huo kuomba msaada wa huduma ya kwanza, kabla ya kupelekwa hospitali ya Mnazi Mmoja kwa matibabu.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Mkadam Khamis Mkadam, alisema maji hayo yamemuathiri Padre Mwang’amba usoni, kifuani, mikononi, mapajani na kuchoma sehemu kubwa ya mbele ya nguo yake.
Akizungumza na NIPASHE Jumamosi kutoka Zanzibar, Mkadam, alisema Padre Mwang’amba ana tabia ya kwenda kwenye mgahawa huo mara kwa mara, kwa ajili ya kusoma na kutumia mtandao wa `intaneti’.
Alisema katika kwenda na kupata huduma hiyo mahali hapo, hakuna taarifa za kuwapo kutoelewana ama vitisho vya aina yoyote dhidi yake.
“Alipomwagiwa maji hayo, alikuja mwenyewe kituo cha polisi Mji Mkongwe kutoa taarifa, lakini polisi haikumhoji zaidi kwa sababu alitakiwa kukimbizwa hospitali kupata matibabu,” alisema na kuongeza kuwa hatahojiwa mpaka atakapopata nafuu.
Alisema wakati akifika polisi, hakuonyesha dalili za kuathirika hali ambayo ilikuwa tofauti baada ya kufikishwa hospitalini na kwamba hadi kufikia jana jioni, hakuna mtu aliyekamatwa.
Mkadam alisema Padre huyo anatoa huduma katika parokia ya Machui iliyoko eneo la Cheju mjini hapa.
Habari zaidi kutoka Zanzibar zilieleza kuwa Mwang’anda anahudumia kituo cha malezi ya vijana cha Cheju kinachoendeshwa na kanisa hilo.
Hili ni tukio la tano la kumwagia tindikali hapa Zanzibar katika mashambulio yaliyotokea kati ya mwaka jana na mwaka huu .
Katika tukio la kwanza Mkurugenzi wa Manispaa ya Zanzibar Rashid Ali Juma, alimwagiwa tindikali na baadaye Katibu wa Mufti Sheikh Fadhil Suleiman Soraga alijeruhiwa na kemikali hiyo.
Wengine waliomwagiwa tindikali kwa nyakati tofauti ni Sheha wa Chumbuni, Mohamed Kidevu wakati mwezi Julai wasichana wawili wa Uingereza Katie Gee (18) na Kirstie Trup, walimwagiwa kemikali hiyo.
Wasichana hao waliokuwa wanajitolea kufundisha katika shule moja mjini hapa, walishambuliwa baada ya tukio la kumwagiwa tindikali Katibu wa Mufti wa Zanzibar, Sheikh Fadhili Suleiman Saroga.
Kwa upande wa mashambulio dhidi ya viongozi wa Kanisa Katoliki kujeruhiwa, Padri Mwang’amba ni mfululizo wa matukio hayo yaliyoanza na kushambuliwa Ambrose Mkenda, alijeruhiwa kwa kupigwa risasi, wakati wa Sikukuu ya Krismasi, mwaka jana.
Tukio hilo lilifuatiwa na mauaji ya Padri Aloyce Mushi, aliyeuawa kwa kupigwa risasi Februari mwaka huu, wakati akielekea kwenye ibada ya Jumapili saa 1:00 asubuhi.

CHANZO: NIPASHE
3 comments:
Hizo gharama za kuwajulia hali wagonjwa kwanini zisitumike kuwakama wahalifu wa tindikali. Kikwete naye ataenda siyo muda mrefu kuanzia leo. Kama meshindwa kuwakamata ombeni msaada wa intel kutoka nje.
TINDIKALI na Zanzibar ni kama Pete na kidole!!!!!!! Zanzibar imekuwa uwanja wa mauaji!!!! UGAIDI unatingisha Zanzibar!!!! Wanamwagia Kila mtu asiye muisilamu Tindikali!!!! Na Kama hufananiii ki Zanzibar pia unamwagiwa TindiKAli !! mie naona Watu waa ache kabisaa Kwenda ZAnzibar uone jinsi uchumi wa nchi hiyo utakavyo yumba!!! Na watali pia waigomee Zanzibar ..
Hamna kitu hapo, hiyo ni danganya toto tu! Haya mambo ya kuficha uozo yana mwisho wake; utamwagia tindikali wengine baadae itafika ndani kwako. Ina maana toka shughuli za tindikali zimeanza hakuna mtu anayejua kitu chochote - wanagapi wametuhumiwa?
Post a Comment