ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, September 25, 2013

KINANA AMALIZA ZIARA YAKE MKOA WA MARA KWA MAFANIKIO

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Musoma mjini kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Mkendo.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Musoma mjini katika viwanja vya shule ya msingi Mkendo.
 Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana akipokea zawadi ya sanamu ya mfano wake kutoka kwa Ndugu Elia Bugurilo Kamoga.


Josephat Amon Muruga akiwa na wenzake sita baada ya kujiunga na CCM wakitokea Chadema.


Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa anavuka na kivuko cha MV Musoma kutoka Kinesi kuelekea Musoma mjini,Kivuko hicho ambacho kimekuwa  mkombozi  wa usafiri kinauwezo wa kubeba abiria 330.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akijaribu vazi la kujiokoa wakati wa hatari wakati wa kuvuka  na kivuko cha MV Musoma.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishangiliwa na Balozi wa shina namba 6 Tabitha Edgar wa kata ya Kitagi.
Balozi wa nyumba kumi Tabitha Edgar wa shina namba 6 kata ya Kitagi akitoa shurani zake za kutembelewa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abbulrahman Kinana.
Katibu Mkuu akipata maelezo ya ujenzi wa mradi wa maji kutoka ziwa Victoria uliopo eneo la Bukanga(Makoko) mradi huo utakamilika katikati ya mwaka ujao.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  akikagua maendeleo ya mradi mkubwa wa maji huku akipatiwa maelezo na mhandisi Jairos Chilema ,mradi huo utakuwa na bomba kubwa la kilomita tisini na ukikamilika utaondoa kabisa tatizo la maji Musoma Mjini.
  • AFANYA ZIARA MUSOMA MJINI
  • ATEMBELEA MRADI MKUBWA WA MAJI
  • ASEMA WANANCHI WANAHAKI YA KUHOJI MAENDELEO YAO
  • AWATAKA WANANCHI KUTAMBUA MASUALA YA MSINGI YANAYOWAHUSU
  • ZAIDI YA VIONGOZI SITA KUTOKA UPINZANI WAJIUNGA CCM

1 comment:

Anonymous said...

ZAWADI umepata tena nzuri sana na umeikubali. Huyu ndugu kwa upendo wake mwenyewe bila kutumwa alichukua muda wake mwingi tu kuiandaa! Je unapooza kidogo dogo chochote? kwanza muangalie anachotumia kumudu maisha yake ya kila siku ni nini? na wako wangapi. Isije ikawa mmeuza tu siasa hapo, na huyu ndugu yangu N.P anaangalia, je upo hapo? Siasa na wtu wake.