Wanahabari wa vyombo mbali mbali na wadau wa habari mkoa wa Iringa wakiwa katika maandamano ya amani ya kumuenzi aliyekuwa mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IPC) leo
Maandamano ya wanahabari na wadau wa habari yakipita eneo la soko kuu la manispaa ya Iringa
katibu wa IPC Francis Godwin akiongoza maandamano ya wanahabari na wadau huku akiwa juu ya gari na picha ya marehemu Daudi Mwangosi
Wanahabari Iringa katika maandamano ya kumuenzi marehemu Mwangosi leo
Maandamano ya wanahabari na wadau wa habari mkoa wa Iringa ya kumuenzi marehemu Daudi Mwangosi yakipita eneo ya uhindini
(picha na habari kwa hisani ya Francis Godwin.)
Wananchi wakishuhudia maandamano hayo leo
katibu mtendaji wa IPC Francis Godwin akitoa taarifa ya kuanza kwa maandamano ya kumuenzi marehemu Daudi Mwangosi leo
Katibu wa IPC Francis Godwin mwenye pama akikabidhi maandamano ya mwenyekiti wa IPC Frank Leonard na wadau wengine eneo la Maktaba ya mkoa wa Iringa
Katibu wa IPC FrancisGodwin kushoto akikabidhi picha ya marehdemu Daudi Mwangosi kwa mwenyekiti wa IPC Frank Leonard kulia,wanaoshuhudia ni mzee Fulgence Malangalila na Majid Mjengwa
Mwenyekiti wa IPC Frank Leonard kushoto akikabidhi picha ya Mwangosi kwa mwasisi wa IPC mzee Fulgence Malangalila
Viongozi wa IPC kutoka kulia Francis Godwin katibu na Frank Leonard mwenyekiti na mwakilishi wa wananchi
MAANDAMANO ya wanahabari mkoa wa Iringa kwa ajili ya kumbukumbu ya mwaka mmoja ya kifo cha aliyekuwa mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IPC) na mwandishi wa Chanel Ten Marehemu Daudi Mwangosi yatikisa mji wa Iringa leo
Maandamano hayo ambayo yameanza majira ya saa 4 asubuhi katika viwanja vya bustani ya Manispaa ya Iringa yamepita kuzungu kakatika maeneo mbali mbali ya mji wa Iringa kabla ya kupokelewa na mwenyekiti wa IPC Frank Leonard katika ukumbi wa maktaba ya mkoa kwa mkutano wa wadau wa habari.
Maandamano hayo yamepita maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na eneo la Uhindini , Mashine tatu, Soko kuu na stendi kuu ya mabasi ya mikoani wananchi walilazimika kusitisha shughuli zao kushuhudia maandamano hayo ambayo yaliongozwa na askari wa usalama barabarani.
Akizungumza baada ya kupokea maandamano hayo ,mwenyekiti wa IPC Bw Leonard alisema kuwa lengo la maandamano hayo ni kumkumbuka Mwangosi pamoja na kutazama changamoto mbali mbali ambazo wanahabari wamekuwa wakikabiliana.
Alisema kuwa hakuna mtanzania asiyetambua mchango wa Mwangosi katika uhai wake na kuwa kutokana na mchango wake umoja wa vilabu vya waandishi wa habari Tanzania (UTPC) umeanzisha tuzo maalum kwa wanahabari itakayopewa jina la Daudi Mwangosi na mshindi atapewa kiasi cha Tsh milioni 10.
Alisema tuzo hiyo itakuwa ikitolewa kila mwaka na UTPC na ili mwanahabari aweze kushinda tuzo hiyo ,lazima apitie katika misuko suko katika kazi hiyo ,pia wale watakaopigania maslahi yao na fisa nyingine nyingi.
Hivyo aliwataka wanahabari wanachama wa Vilabu vya wanahabari na wale wasio wanachama ambao wanafanya kazi Tanzania kujitokeza kuchangamkia tuzo hiyo.
Mbali hilo aliwataka wanahabari kuendelea kuzingatia maadili yao ya kazi hiyo ili kuongeza imani kwa watanzania .Alisema kuwa wapo wanahabari watafanya watazingatia maadili ya uandishi Taifa linaweza kupiga hatua katika maendeleo.
Wakati huo huo IPC imetoa mikopo ya zaidi ya Tsh 500,000 kwa wanachama wake ili kuwawezesha kuboresha zaidi shughuli zao kwa kununua vifaa vya kazi.
Marehemu Mwangosi aliuwawa na polisi septemba 2 mwaka 2012 katika kijiji cha Nyololo wilaya ya Mufindi wakati wa ufunguzi wa tawi la Chadema kijiji cha Nyololo.
No comments:
Post a Comment