Hii ni kampuni mpya mitindo ambayo imeanza kupamba moto toka mwishoni mwa mwaka jana chini ya designer JOCKTAN WA MAKEKE AFRIKA pamoja na SCHOLASTICA WA MAKEKE AFRIKA na kutwaa umaarufu wa kutosha kutokana na kazi zake kutokea kuwakuna sana wapenzi wengi wa mitindo nchini Tanzania na hata nje pia, Mitindo hio ya ki – makeke inazidi kuchanja mbuga kwa spidi ya ajabu kwani ina mahadhi ya mwafrika halisi na cha kushangaza zaidi ni kwamba makeke afrika koleksheni imezidi kuboresha muonekano wake na kuwa wa mvuto zaidi na wamezidi kuboresha huduma kwa wateja wao, hawa jamaa pia ndio waanzilishi wa mitindo ya ki – makeke na show ya Rangi Rangi za Makeke(RRM) Fashion wikend ambayo imefanya vizuri sana na kupokelewa vzuri na mashabikiwa mitindo Tanzania
kwa picha zaidi bofya soma zaidi
No comments:
Post a Comment