ANGALIA LIVE NEWS

Monday, September 16, 2013

MAKOSA 10 WANAUME HUYAFANYA WAKIWA FARAGHA -3

KARIBU msomaji wangu tuendelee na mada yetu. Wewe ni mwanaume hutakiwi kufanya haya makosa ambayo nayaelekeza. Hii itakusaidia kuboresha uwezo wako faragha.

Kosa la kwanza nililieleza wiki iliyopita kuwa wanaume hukosea kwa kudhani wanawake wanaridhika na huduma wanayopewa faragha wakati siyo kweli. Tumia uanaume wako kutegua kitendawili hiki.
Wanawake wana utani sana, anaweza kuangusha mayowe na kujitikisa kuonesha namna anavyosisimka kumbe hamna lolote. Anaweza kulia kwa sauti ya juu kwamba anafika kileleni wakati siyo kweli. Hufanya hivyo ili kukufurahisha wewe mwanaume.
Wanajua kwamba wanaume hujiona wapo ngangari pale wanapo-wafikisha wanawake wao kileleni. Sasa basi, ikitokea mchezo anaona ni mrefu na hafurahii chochote, huamua kuifanya mechi ifike tamati kwa kudanganya amefika kileleni kisha anamtaka na mwanaume wake naye amalize.
Soma mawazo haya ya mwanamke huyu ambaye ni msomaji wangu: “Kuna maeneo ambayo mwanaume wangu akiyagusa ndipo nafika kileleni. Katika wanaume niliowahi kukutana nao, wote wana staili moja. Hawanipatii.
“Sasa, ninapoona mwanaume anakuwa hanifikishi kule ninapohitaji, dawa pekee huwa ni kujifaya napata raha na baadaye namwambia nimefika kileleni, baada ya hapo naye namwambia amalize. Huwa nafanya hivyo kwa sababu sioni kitu kipya.”
Ni kweli kwamba wanawake wengi huwa wanafiki wakiwa faragha. Wewe unatakiwa ulijue hilo na usikubali kudanganywa. Unapogundua mambo hayapo sawa, badili uelekeo kisha nenda kivingine mpaka uone anapata msisimko wa kweli.
Kwa kawaida mwanamke huwa anahitaji mazungumzo kwanza. Cheza naye hapa na pale, zungumza naye kimahaba. Kama una stori za kuchanganya kichwa, msimulie. Ni kosa kubwa sana kuanza mchezo bila kumtongoza. Ni mwenzi wako na tayari mpo chumbani, ila mtongoze tena ili umpe sababu ya kufanya hicho kitendo.
Toa ahadi kwake kwamba siku hiyo umemwandalia penzi zuri litakalomfanya afurahi kuliko nyakati nyingine zote. Zungumza hivyo ili umvutie, umsisimue kisha mwenyewe akukumbatie. Maneno yako yatamfanya yeye alainike mpaka barabara yake iwe teketeke kabla hata hujamgusa popote.

HUTOI MITINDO NA UZOEFU MPYA
Kuna wanaume wenye kasumba ya kukariri. Pengine ni mgeni katika mapenzi, kwa hiyo hawezi kubadilika kutokana na mazingira au kulingana na mwanamke aliyenaye. Kipengele hiki kinawafelisha wengi. Wanapoteza sifa na alama ambazo zingewafanya waonekane wapo juu faragha.
Ulipoanza tu kuyajua mapenzi, ukakutana na mwanamke ambaye alikwambia mtindo anaoufurahia ni kibodaboda, nawe kwa kukosa ubunifu, unadhani kila mwanamke anafurahi kupandishwa pikipiki. Unakosea, kila mwanamke ana kipawa chake na wigo wake katika mapenzi.
Mwanaume hutakiwi kuwa na papara, badili mitindo kwa utaratibu unaofaa, kila hatua utakayovuka, hakikisha upo pamoja na mwenzi wako, kwa hiyo mawasiliano na majadiliano ya hapa na pale ni muhimu sana katikati ya kitendo.
Hapa labda nifafanue kwamba majadiliano ambayo nayasema hapa ni yale yanayohusu kitendo. Sina maana ya maongezi yoyote yale. Imebidi niliweke hili wazi kwa sababu kuna uwezekano mkubwa wa mtu kuanzisha mazungumzo ya pembeni halafu akasema Luqman alishauri.

Itaendelea wiki ijayo.

GPL

No comments: