ANGALIA LIVE NEWS

Friday, September 27, 2013

Polisi waliotimuliwa walalamika


Askari 15 wa Jeshi la Polisi nchini wanaodaiwa kufukuzwa kazi Juni mwaka huu, wamelalamikia kuvunjiwa nyumba zao na kuondolewa kwa nguvu na vyombo vyao kutolewa nje ilhali bado hawajapewa barua rasmi za kufukuzwa kazi kutoka makao makuu ya jeshi hilo.

Kati ya askari hao watatu wanaishi katika kambi ya Kunduchi na wengine wanaishi nyumba za polisi Magomeni na wengine wanaishi katika nyumba za uraiani, walifukuzwa kazi kwa kile kilichodaiwa kuwa walikamata mafuta ya chakula ya magendo yaliyokuwa yanapitishwa kinyemela kupitia bandari ya Bagamoyo yanayodaiwa ni ya kigogo mmoja.

Aaskari hao walisema juzi alfajiri walikuja askari waliojitambulisha kuwa wametoka makao makuu ya Jeshi la Polisi kuwataka waondoke katika nyumba hizo na kuvunja mlango wa PC Bahati Mziba na kutoa vitu vyake nje bila ya kuwa na barua yoyote.


Kwa mujibu na hukumu na mwenendo wa kesi iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni Juni 6, mwaka huu kwa shitaka la kufanya kitendo kinyume na mwenendo wa Jeshi la polisi Tanzania K/FC.5 (XLVII) cha PFSR, 1995

Waliofukuzwa kazi ni F.1800 Sgt Hemed, D.8137D/Cpl Julius, E.2653Cpl Leonard, E.4565 Cpl Halifa, E.Cpl Methord, E.6798 Cpl Omary, E.7897Cpl Kasigara, F.1829 PC Bahati, F.8399 PC Mihayo, F.8939PC Peter, F.9900 PC Hamisi, G.471PC Shaibu, G.111 PC Stanford, G.4400 PC Awadhi na WP.4850 PC Mtumwa huku wengine wanne wakihamishwa vituo vyao vya kazi.

“Inatakiwa tupewe barua za kufukuzwa kazi ndipo waanze utaratibu wa kutuambia tuhame katika nyumba zoezi hilo liende sambamba na kupewa mafao yetu,” alisema PC Bahati.

Kwa mujibu wa hukumu hiyo ambayo NIPASHE imeiona, kuwa vitendo walivyofanya askari hasa hasa wale walionekana wazi kwenye VCD wakipokea au kugombea kupokea fedha kutoka kwa mfanyabiashara na kuwa ni vitendo vya kulitia aibu na kulifedhehesha Jeshi la Polisi.

Mkuu wa Kitengo cha Sheria Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, Kamanda Mwauzi, alisema barua zao za kufukuzwa kazi ziko tayari na wanatakiwa kwenda kuzichukua pamoja na utaratibu wa kulipwa mafao yao.

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camilius Wambura, alisema Kambi ya Kunduchi haiko Kinondoni iko Baracks hivyo, wanaotakiwa kulizungumzia hilo ni Kanda Maalum ya Dar es Salaam.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments: