Mkurugenzi wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Steve Gannon akiongea na washindi wa tiketi za VIP kutoka kote nchini(hawapo pichani) baada ya washindi hao kuwasili kwa ajili ya ziara kiwandani hapo, washindi hao watashuhudia tamasha la Serengeti Fiesta kesho jijini Dr es Salaam.
Meneja wa mipango kwa wateja wa kampuni ya bia ya Serengeti Nandi Mwiyombela akiwakaribisha washindi wa tiketi za VIP(hawapo pichani)baada ya washindi hao kutembelea kiwanda cha bia cha Serengeti. washindi wa VIP 75 watanufaika na ushindi huo kwa siku nne hapa jijini Dar es salaam
Ni katika viwanja vya Leaders Club ambapo shamrashamra na maandalizi ya steji pamoja na kuandaa mazingira kwa ajili ya tamasha la Serengeti Fiesta ambalo litafanyika kesho.
baadhi ya washindi wa tiketi za VIP wakitoka kupata chakula cha pamoja katika mgahawa wa Break Point, Makumbusho baada ya kutoka katika ziara ya kutembelea kiwanda cha bia cha Serengeti.
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake