ANGALIA LIVE NEWS

Friday, October 18, 2013

AyoTV Exclusive interview na Ommy Dimpoz baada ya kutoka Marekani

Ni show tatu alizofanya kwenye miji mbalimbali ya Marekani ambayo ni Washington DC, Houston Texas na Hollywood California ambapo hii ni mara ya kwanza kwa Ommy Dimpoz kwenda Marekani lakini ni nchi ya 15 kuitembelea nje ya Tanzania ndani ya mwaka huu peke yake kutokana na muziki wake tu.

Mapokezi

Ommy anakwambia ‘Bongofleva inatupeleka mbali na kututangaza yani unakwenda sehemu, ukiona jinsi unavyopokewa mpaka unasema yani muziki wangu ndio umekua na nguvu kiasi hicho? alafu pia Mapromota wamekuwa waelewa na kutupa umuhimu hata kwenye ndege nimepanda Business Class ambayo siku zote nilikua napapita tu na kwenda kukaa kule kwa kawaida’

Kuhusu malipo ya show:

‘Naweza kusema hapa nyumbani tunalipwa pesa nyingi zaidi kwenye show kuliko kwenye show za nje, nyumbani unaweza kufanya show mbele ya watu hata elfu 10 lakini kule ni show ambayo ina watu wachache ambao mara nyingi ni Watanzania hivyo malipo yanapungua kidogo ndio maana unakuta unalipwa milioni 4, 5, 6 au 7 na mwenyewe ukiangalia mazingira kweli unaona na kuelewa’ – Ommy
Kuhusu kukutana na mwimbaji 2Face wa Nigeria:
‘Yeah alikuja kwenye show yangu, ni kitu ambacho kilinipa faraja… tulikutana mchana nikampa mwaliko wa kuja na akaja kweli akashow love… nilijua ni msanii mkubwa Afrika na nikampa anuani na kweli jamaa akaja usiku sikudhani kama angekuja kweli… nilijua nimempa mwaliko lakini angeipotezea, alikuja hata show yangu haijaanza tukaongea backstage mambo mengi ya kikazi na akasubiri mpaka akaona show yangu… huko mbele tutajua nini kitatokea’ – Ommy

Kitu gani ulikifanya tofauti na show Marekani?

‘Nimefanya video ya wimbo wangu ambao upo lakini pia kulekule nilipata mtu akanitengenezea logo ya PKP yani Poz kwa poz, ni brand yangu ambayo ni Clothing line….. inakuja, jeans, nguo za ndani viatu na kofia

No comments: