Tuesday, October 29, 2013

BONGO MOVIE WAMTENGA WEMA MSIBA WA BABA YAKE.

KATIKA hali isiyotarajiwa katika wasanii wanaounda kundi la Bongo movie wamejikuta wakijitenga kushiriki msiba wa Baba mzazi wa msanii mwenzao Wema Isack Sepetu, baada ya kuundwa zengwe na mmoja wa watu wenye ushawishi katika kundi hilo, Wema akiongea kwa uzuni amesema kuwa hata wale waliofika jana katika msiba huo hawakufika kwa ajili ya kumfariji bali walifika kwa ajili ya kumsanifu. 
FC ilifanya utafiti ili kubaini hilo kwa kuwapigia simu baadhi ya wasanii wanaotoka katika kundi hilo nao bila kusita kwa masharti ya kutotajwa majina walitiririka kwa kusema kuwa ni kweli uongozi wa kundi hilo umetoa agizo watu wasishiriki kutokana na tabia ya msanii huyo kutoshiriki katika misiba ya wasanii wenzake.
“Ni kweli hilo lipo na lina ukweli kwa njia moja au nyingine Wema bwana huwa hashiriki katika misiba ya wasanii wenzake, kuna mtu muhimu sana na ana sauti katika kundi la Bongo Movie amesema kuwa katika misiba iliyotokea ameshiriki misiba miwili tu, wa marehemu Sharo na Kanumba kwa sababu alikuwa mtu wake,”anasema kijana huyo.
Hili si jambo la kulifurahia kwa wasanii kwani halijengi bali linaleta mgawanyiko wa moja kwa moja, msanii mwingine alikiri kuwa Wema anabagua kushiriki misiba kwani wakati amefariki marehemu John Maganga alipigiwa simu ili ashiriki katika msiba lakini alisema yupo Location, hivyo wasanii wenzake wanamtenga ili aone umuhimu wa kushiriki misiba ya wenzake.

Jana jioni nyumbani hakukuwa na wasanii zaidi ya mtangazaji wa kipindi cha Take One Zamaradi Mketema akiwa na Rais wa shirikisho la wasanii Simon Mwakifwamba na waombolezaji wengine, huku baadhi ya wasanii wakifika pale na kuondoka jambo ambalo Wema alilitafsiri kama walifika pale kutoa lawama ili asiwaone kama hawajafika lakini hawakuwa na dhamira ya kweli mioyoni mwao.

7 comments:

  1. Mmmh! Kutokuhudhuria mazishi ya wasaniii wenzaake in kibaya sana maana kuna Leo na kesho ila sioni Kama ku tena Ni solution jamani!!!! Khaaa! Mngemuita chemba na kumweleza tu kuwa tabia yake Ni mbaya na aiache Mara moja! Wema usijali haya yoote Ni maisha tu! Na Rais wa nchi alikuwepo na mke wake kuku support kwa hiyo shukuru hilo wangapi wanamuonaga Rais wa nchi katika msiba??? Ila hata Diamond wako kakutenga pia jamaniii? Wanaume bwana hawaaaminiki kabisa! Yeye alitakiwa kuku support kwenye raha na Shida! Hovyooooooo! Pole sana Wema maisha Ni kujifunza bidada.

    ReplyDelete
  2. Pole sana wema,Mungu pekee ndio anaweza kukupa faraja ya milele hata hao wasanii wasipokuja haikupunguzii kitu, pia na nyie wasanii akili zenu mbovu sana wenzenu 1wakipizana kwenye harusi nyie hadi msibani lol! aibu kwenu, na pia naona mnamuonea wivu wema wetuu mnafikiri ndio mtamchafuliaaa??? she still rock. love yah wema sepetu

    ReplyDelete
  3. kwahiyo nyie wasanii ndio mmefaidika nn kwa kutoenda kwenye msiba wa msanii mwenzenu? hata kama kafanya kosa, ss hapo mtaishi na maguilty yenu na kuanza kumkimbia na mnaosema eti mmeambiwa na mtu mmina mwenye ushawishi mkubwa hamnazo kweli, na wema uachae kucheza mamovie yao, wanakuonea wivu tuu hawana lolote.

    ReplyDelete
  4. Nyinyi mnaemuonea huruma wema na kuwasema wasanii wenzie wamefanya vibaya kutokwenda kwenye msiba kwani hamsomi sababu ni nini? ni yeye ambae ameanza kutoshiriki misiba ya wasanii wenzake kwa kujiona yeye ni star sana eti Raisi ameenda Raisi hakwenda kwa sababu ya wema au mama yake wema Raisi ameenda ni kwa sababu alofariki alikua alishawahi kuwa mfanyakazi wa serikari kwenye nyazifa za juu si kwa sababu ya wema kalaleni kule dawa ya moto si maji ni moto tu

    ReplyDelete
  5. Pole sana Wema . Kwani hao waliojitenga wamekupunguzia nini, Watu wengine bwana . Songa mbele na maisha yako waswahili ndivyo walivyo hawakosi sababu

    ReplyDelete

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake