Gari aina ya Mercedes Benz la Rita Paulsen 'Madam Rita' limeteketea kwa moto likiwa barabarani Jumamosi iliyopita, OKt 26, 2013. Hata hivyo kwenye gari hilo lililozimika barabarani na kuanza kuwaka moto, hakuwemo Madam Rita bali dereva wake, Julius Kanwakaita. Chanzo kilichopelekea gari hilo kuwaka moto hakijafahamika mara moja. Agosti 21 mwaka jana, ofisi za kampuni yake ya Benchmark Productions zilizopo Mbezi Beach jijini Dar ziliteketea pia kwa moto.
CHANZO TIMESFM
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake