Kamanda wa polisi Mkoa wa Tanga Costantine Massawe amesema hili tukio limetokea saa nne na nusu usiku kwenye kijiji cha Shume tarafa ya Mlola ambapo askari huyu aitwae Oforo, amejeruhiwa alipokwenda na wenzake wawili kumkamata mtuhumiwa kutokana na kibali kilichotolewa na Mahakama wilayani humo kufuatia mgogoro wa ardhi.
Walipofika, walitokea watu wawili waliowashambulia askari kwa mapanga kitendo kilichofanya askari huyu kuwafyatulia risasi na kumuua mmoja wao ambae alifariki akifanyiwa matibabu kwenye hospitali ya Lushoto huku aliejeruhiwa akiendelea kupata matibabu.
No comments:
Post a Comment