Mtanzania Gee ambae ni rafiki yake, anasema ‘Alhamisi Elvis alikwenda kumtembelea rafiki yetu mmoja anaitwa Lulu (Sio mwigizaji) anaishi Mbezi Beach Africana ambapo Ijumaa jioni mida ya saa moja alijisikia kwenda kuogelea kwenye swimming pool, Lulu alimwambia asiogelee kwa sababu ilikua usiku umeshaingia lakini Elvis aliiamua kuogelea hivyohivyo’
‘Lulu alitoka nyumbani kidogo wakati huo Mac akienda kuogelea akiwa mwenyewe, ilikua ni kawaida kwake kuogelea mara nyingi huwa anapenda kuogelea hivyo hakikua kitu kigeni… Lulu aliporudi hakumuona Mac manake hakurudi hivyo akadhani mwimbaji huyu ameshaondoka, akawa anampigia simu rafiki anaeishi na Mac lakini haikupokelewa’ – Gee
No comments:
Post a Comment