Brass Band ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ikiongoza Matembezi ya Hisani kwa ajili ya Harambee ya Kuchangisha fedha za Ujenzi wa Shule za Sekondani za Kata katika Tarafa ya Mbagala,iliyofanyika katika Uwanja wa Shule ya Sekondari ya Mt. Anthony,Mbabala jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.Mgeni Rasmi katika Harambee hiyo ambayo iliambatana na Uzinduzi wa Mahafali ya Wanafunzi wahitimu wa Kidato cha Nne alikuwa ni Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa.ambapo zaidi ya shilingi milioni 250 zilipatikana kwenye harambee hiyo.
Baadhi ya Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakipiga vyombo mbali mbali vya Muziki kwenye Matembezo hayo.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (katikati) ambaye ndie aliekuwa Mgeni Rasmi kwenye harambee hiyo akionekana kwenda sambamba na Matembezi hayo.
Mh. Lowassa akiwasalimia Wanafunzi,Walimu na Wazazi wa Watoto wanaosoma katika Shule mbali mbali za Sekondari eneo la Mbagara jijini Dar es Salaam leo.
Sehemu ya Wanafunzi kutoka Shule mbali mbali za Kata zilizopo kwenye Tarafa ya Mbagala jijini Dar es Salaam wakimsikiliza Mgeni Rasmi,Mh. Edward Lowassa (hayupo pichani).
Mwanafunzi wa Kidato cha Kwanza wa Shule ya Sekondari ya Mbagala jijini Dar es Salaam,Kijoy Selemani akisoma Risala ya Wanafunzi kwa niaba ya Wenzake wa Shule mbali mbali zilizopo katika Tarafa ya Mbagala jijini Dar es Salaam,wakati wa Harambee ya Kuchangisha fedha za Ujenzi wa Shule za Sekondani za Kata katika Tarafa ya Mbagala iliyoenda sambamba na Uzinduzi wa Mahafali ya Wanafunzi wahitimu wa Kidato cha Nne,iliyofanyika katika Uwanja wa Shule ya Sekondari ya Mt. Anthony,Mbabala jijini Dar es Salaam
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiteta jambo na Mbunge wa Jimbo la Kigamboni,Mh. Dkt. Faustine Ndugulile muda mfupi kabla ya kuanza kwa harambee hiyo.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mbagala,Mwl. Marcelina Kimario akisoma risala mbele ya Mgeni Rasmi kwenye Harambee hiyo.
Mbunge wa Jimbo la Kigamboni,Mh. Dkt. Faustine Ndugulile akiwahutubia Wananchi wa Mbagala pamoja na Wanafunzi wa Shule mbali mbalia zilizopo kwenye Tarafa ya Mbagala,wakati wa Harambee ya Kuchangisha fedha za Ujenzi wa Shule za Sekondani za Kata katika Tarafa ya Mbagala iliyoenda sambamba na Uzinduzi wa Mahafali ya Wanafunzi wahitimu wa Kidato cha Nne,iliyofanyika katika Uwanja wa Shule ya Sekondari ya Mt. Anthony,Mbabala jijini Dar es Salaam
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwahutubia Wananchi wa Mbagala pamoja na Wanafunzi wa Shule mbali mbalia zilizopo kwenye Tarafa ya Mbagala,wakati wa Harambee ya Kuchangisha fedha za Ujenzi wa Shule za Sekondani za Kata katika Tarafa ya Mbagala iliyoenda sambamba na Uzinduzi wa Mahafali ya Wanafunzi wahitimu wa Kidato cha Nne,iliyofanyika katika Uwanja wa Shule ya Sekondari ya Mt. Anthony,Mbabala jijini Dar es Salaam.ambapo jumla ya Sh. Mil 250 zilipatikana kwenye harambee hiyo.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akisalimina na Mbumbe wa Jimbo la Ilala,Mh. Mussa Azan Zungu.
Wananchi wa Mbagala wakionyesha moyo wao wa kuchangia elimu katika Tarafa yao,mbele ya mgeni rasmi.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akizungumza jambo na mmoja wa wakazi wa Mbagala aliejitambulisha kwa jila la Bi. Aisha.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akikabidhi vyeti vya kuhitimu elimu ya Sekondari kwa wanafunzi wa Kidato cha Nne kutoka shule mbali mbali zilizopo kwenye tarafa ya Mbagala jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Madiwani wa Temeke wakiwa kwenye Harambee hiyo.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (katikati) akipokea zawadi kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Harambee hiyo,Bw. Tryphon Lutina (kushoto) mara baada ya kumalizika kwa harambee hiyo.Kushoto ni Mbumbe wa Jimbo la Kigamboni,Mh. Dkt. Faustine Ndugulile.
Picha ya Pamoja na wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya harambee hiyo.
Mh. Lowassa akiwaafa wakazi wa Mbagala.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiagana na Mbunge wa Jimbo la Kigamboni,Mh. Dkt. Faustine Ndugulile.
Picha na Michuzi
2 comments:
Asane sana kwa hisani ya harambee. Basi mheshimiwa wahimize wananchi na wasamaria wema, tunao matajiri wengi sana nchini Tanzania nahasa Jijini Dar Es Salaam! Hebu tizama hao watoto wapendwa mbele yako wamekaa chini kwenye dongo, kweli tunashindwa kununua hata viti vya plastic ambavyo ni rahisi kuwakalisha. Waandaaji mnapoandaa shughuli muhimu kama hizi tuondoe aibu jamani. Hongereni.
Aliyekuwa Waziri Mkuu awamu ya kwanza ya Serikali ya mh. Kikwete, Na sio waziri mkuu MSTAAFUUUUUUUUU!!
Post a Comment