Miss Universe Tanzania 2013 Betty Boniface Omara (kushoto) akikabidhiwa bendera na Waziri wa Maliasili na Utalii Mheshimiwa Khamis Kagasheki (kulia) katika ukumbi wa mkutano wa wizara hiyo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkurugenzi wa Kitaifa Miss Universe Tanzania Maria Sarungi Tsehai.
PRESS RELEASE
Mrembo wa Miss Universe Tanzania 2013 Betty Boniface Omara amekabidhiwa bendera leo na Waziri wa Maliasili na Utalii Mheshimiwa Khamis Kagasheki.
Zoezi hili limefanyika katika ukumbi wa mkutano wa wizara hiyo tayari kwa safari yake ya kwenda kwenye mashindano ya Miss Universe yatakayofanyika Moscow nchini Urusi mapema mwezi Novemba.Mrembo wa Miss Universe Tanzania 2013 Betty Boniface Omara amekabidhiwa bendera leo na Waziri wa Maliasili na Utalii Mheshimiwa Khamis Kagasheki.
Akimkabidhi bendera huku akimpongeza Waziri Kagasheki pia amemtakia mafanikio mema huko aendako.
Betty pia aliwaahidi Watanzania kuwa mbali na kurudi na ushindi lakini pia ataenda kuitangazia dunia kuacha kutumia nakshi (Mapambo) yanayotumia pembe za ndovu ili kumaliza tatizo la ujangili nchini.
Zoezi la kukabidhiwa bendera lilifanyika likishuhudiwa na Mkurugenzi wa Kitaifa Miss Universe Tanzania Maria Sarungi Tsehai.
Mashindano ya Miss Universe Tanzania 2013 yamedhaminiwa na Hifadhi ya Taifa Tanapa na Mrembo Betty Boniface ameshaanza kutangaza hifadhi hizi kwa njia mbalimbali hapa nchini na nje ya nchi.
No comments:
Post a Comment