ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, October 26, 2013

Msiba wa Martha Shani DC na mapambano dhidi ya uvutaji sigara nchini Marekani

Katika kipindi cha DAKIKA 90 ZA DUNIA wiki hii... Kutoka nchini Marekani, tuanze na habari za msiba ulioikumba jamii ya waTanzania waishio maeneo ya Washington DC.
Marehemu Martha Shani
NA KISHA......
Uvutaji sigara, ni sababu kubwa ya vifo vinavyozuilika nchini Marekani. Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Kituo cha Kudhibiti Maradhi nchini Marekani (CDC) kifo kimoja kati ya vitano nchini Marekani hutokana na athari za uvutaji sigara, na zaidi ya watu milioni 43.8 nchini humo ni wavutaji wa sigara.
Lakini vita dhidi ya uvutaji huo vimekuwa vikipamba moto, na teknolojia imekuwa ikishirikishwa katika vita hivyo. Na ni vita hivyohivyo dhidi ya uvutaji vinavyoanza kutiliwa mashaka nchini humo.

Hii ni sehemu ya ripoti ya Jamii Production kwenye kipindi cha DAKIKA 90 ZA DUNIA kinachorushwa na kituo cha Radio cha Capital FM cha Dar Es Salaam Tanzania kila Jumamosi kuanzia saa moja na nusu asubuhi (7:30 AM).

Hii ilikuwa ripoti ya Oktoba 26, 2013

No comments: