ANGALIA LIVE NEWS

Monday, October 28, 2013

MSIBA WA MARTHA SHANI NI MSIBA WA KIPEKEE AMBAO HAUJAWAHI KUTOKEA HAPA DMV.

Kwanza ningependa kwa kuanza kuwapongeza Watanzania wenzangu ndani na nje ya DMV walioshiriki kwenye msiba wa Mtanzania mwenzetu aliyefariki ghafla siku ya Jumamosi Oct 19, 2013 nyumbani kwake Frederick, Maryland baada ya kurudi toka kazini asubuhi ya siku hiyo.

Pili natoa pongezi kwa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani kwa ushirikinao wa karibu waliotoa kwenye msiba huu husuani Balozi Liberata Mulamula kwa moyo wake wa upendo na mshikamano aliouonyesha kama Mtanzania na mwanajumuiya wa DMV kuwa karibu na msiba huu tangia siku uliotokea na kuwaongoza wafanyakazi na maofisa kuchangia na hatimae kununua tiketi tatu za ndege na hatimae kuwasafirisha mume na watoto wa marehemu kwa mazishi ya mpendwa wao Tanzania.


Tatu napenda kuwapongeza NSSF bima ya WESTADI pamoja na kwamba marehemu wala mume wake hawakuwa wanachama wa bima hii lakini wao kwa kujari na kujaribu kuwapunguzia mzigo Watanzania waliokuwa wanaumiza vichwa usiku na mchana kujaribu kufanya kila linalowezekana ili kuwezesha kupata fedha zitakazowezesha kumsafirisha Mtanzania mwenzetu Tanzania kwenye nyumba yake ya Milele. NSSF kupitia bima yake ya WESTADI walituma $5,000/=. NSSF tunawapongeza sana kwa moyo wenu wakusaidia Watanzania tulionje na nyumbani mara tupatapo msiba kama huu wa Martha Shani na hii sio mara yenu ya kwanza kufanya hivyo tua washukuru sana.

Nne ni jinsi msiba huu ulivyokuwa na watu wengi waliojitokeza kwenye kamati ya msiba kawaida ya msiba mingi inapotokea mara nyingi utakuta ni ndugu, jamaa na marafiki wa karibu na familia ya marehemu ndio wanao kuwa wnakamati lakini kwenye msiba huu wa Martha Shani watu wengine waliojiunga kwenye kamati ya mazishi hawajawahi kukutana na marehemu wala familia yake hata siku moja lakini kutokana na kuguswa na msiba huu kama walivyoguswa Watanzania wengine ndio maana ya wao kujitokeza kwenye kamati hii ya mazishi kujaribu kusaidia na hatimaye wamewezesha kumsafirisha marehemu Tanzania kwa mazishi.

Tano ni jinsi msiba huu ulivyokuwa na watu wengi, kawaida ya misiba mingi ambayo imekwishatokea hapa DMV mahudhurio ya watu inategemea na ujulikano wa marehemu au familia yake na yeye alivyokua akijichanganya na Watanzania wengine na muda gani yupo nchi hii. Lakini msiba huu ni tofauti kwa sababu marehemu na familia yake wamekuja Marekani mwaka 2010 na eneo wanaloishi halina Watanzania wengi wanaoishi huko na marehemu alikua ajichanganyi na watu kutokana na muda mwingi alikua mchapakazi.

Mwisho nawapongeza Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV Bwn. Iddi Sandaly akiwemo Makamu wa Rais Bwn Raymond Abraham na Katibu wa Jumuiya ya DMV Bwn. Amos Cherehani bila kuwasahau Watoa habari wa DMV, Changamoto Yetu Blog, Swahili Villa Blog, Sunday Shomari Blog, Swhili TV Blog, Je huu ni uungwana ikiwemo Blog ya Vijimambo kwa ushirikiano na mshikamano wakaribu mliouonyesha kwenye msiba huu.

Kwa sababu hizo tano ndio maana nauita msiba huu ulikuwa wakipekee na wenye mvuto wa aina yake kwani kila aliyeusikia ulimgusa sana bila kujali ujulikano wa marehemu au familia yake na anakotokea kwani ninakumbuka misiba kadhaa ilishatokea hapa DMV na majimbo mengine ilivyoleta shida katika ukusanyaji michango ya mazishi mpaka mingine ilifikia kufanya harambee zaidi ya moja na bado ilishindikana kufikia malengo yaliyowekwa. Mfano hai ni ule msiba wa mpndwa wetu Macrina Joseph Samaka uliotokea July 31, 2011 hapa DMV jinsi gani kamati ilivyohangaika kupata fedha za kumsafirisha marehemu Tanzania ilichukua zaidi ya wiki tatu kuhangaika kuchangisha huku na kule japo baadae kamati ilifanikiwa ikiongozwa na dada ya marehemu aliyekuja toka Tanzania kuchukua mwili wa marehemu.

Kwa hiyo ndugu zangu Watanzania ndio maana waliosema muache Mungu aitwe Mungu hawakukosea hata kidogo na ndio maana nasema Msiba huu wa Martha Shani ulikua msiba wa kipekee ambao haujawahi kutokea hapa DMV uliwowza kukusanya fedha za mazishi zilizovuka malengo. Fedha zilizohitajika ni 16,500 fedha zailizochangishwa zilifikia zaidi ya 21,000.

Bwana ametoa, Bwana ametwaa najina lako lihimidiwe. Amin

5 comments:

baraka daudi said...

Mkuu Dj Luke job well done. Very good written article. Asante sana kwa mchango wako.

Anonymous said...

kweli Mungu mkubwa.

Anonymous said...

wamtumainio bwana ni kama mlima sayuni hawatatikisika milele daima.

Anonymous said...

Spelling errors nyingi sana. Fanya uhariri wa lugha na herufi kabla ya ku post . Pili kuzikana ni kusitiriana, watu waliopita na ugumu wa mazishi Yao haina haja ya kuwataja kwa majina katika shukurani za mazishi ya mtu mwengine,Unakuwa unawasimanga. PAMOJA KATIKA UTANZANIA WETU.

Anonymous said...

Pamoja na nia nzuri ya mwandishi, nadhani ni muhimu makala kama hizi zikafanyiwa uhariri kabla ya kuchapishwa. Pointi ya tano ya "kutojichanganya na watu" haiwezi kuhusishwa na "uchapa kazi" wa mtu, kwa sababu wako watu wengi ambao ni wachapa kazi na bado wanajichanganya kwenye shughuli za watu wengine katika jamii. Pia kulinganisha kifo kimoja na kingine kwa kutaja majina siyo busara. Wale wafiwa waliotajwa kwa lugha ya kejeli "wanastahili kuombwa radhi. Twende shule za uandishi wa habari au tutumie huduma ya kitaalamu ya wahariri!