Wednesday, October 30, 2013

MWANAFUNZI ALIYEPATA UJAUZITO KUTOKANA NA KUBAKWA AOMBA AFANYE MTIHANI WA KIDATO CHA NNE

Joyce Kiria akiwa amembeba mtoto wa Emma.
Joyce Kiria akizungumza na Emma.
Vitendo vya ubakaji vimeendelea kuumiza akili za wapigania haki na ustawi wa wanawake nchini Tanzania kwa muda mrefu sasa. Miongoni mwa kesi hizi zimehusisha wasichana wadogo wenye malengo makubwa katika maisha yao, lakini kutokana na mfumo uliopo, jamii hushindwa kutoa…
Joyce Kiria akiwa amembeba mtoto wa Emma.
Joyce Kiria akizungumza na Emma.

Vitendo vya ubakaji vimeendelea kuumiza akili za wapigania haki na ustawi wa wanawake nchini Tanzania kwa muda mrefu sasa. Miongoni mwa kesi hizi zimehusisha wasichana wadogo wenye malengo makubwa katika maisha yao, lakini kutokana na mfumo uliopo, jamii hushindwa kutoa msaada kwa wahanga wa matukio hayo ili wafanikishe malengo yao.

Emma Roberts ni binti mwanafunzi aliyekumbwa na mkasa wa kufukuzwa shule kutokana na ujauzito alioupata baada ya kubakwa. Kupitia kipindi cha Wanawake Live kinachorushwa na East Africa Television kila Jumanne saa tatu usiku, binti Emma anaelezea tamaa yake ya kufanya mtihani mwezi Novemba, kwa kuwa anaamini kuwa elimu itamsaidia yeye na mwanaye ambaye atalelewa bila kuwa na baba. Kitendo cha kufukuzwa shule kwa tukio kama hili kumemuathiri kwa kiasi kikubwa, na sasa ana hofu ya kutimia kwa malengo yake hapo baadae. Tembelea www.wanawakelivetv.com kwa taarifa zaidi, picha na video.

Kumnyima fursa hiyo ya kuendeleza elimu yake ni kutengeneza taifa lenye wanawake wasio elimu na masikini. Kitendo kilichomkuta Emma, kinaweza kuwakuta wasichana wengi nchini Tanzania. Kuna wale waliojitokeza hadharani, lakini vipi kuhusu wale walioamua kukaa kimya?

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake