Friday, October 25, 2013

RAIS KIKWETE AZINDUA AWAMU YA NNE UTAFUTAJI WA MAFUTA BAHARINI,JIJINI DAR LEO

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akibonyeza kitufe kuashiria Uzinduzi wa Mkutano wa Nne wa Kugawa Vitalu vya Utafutaji Mafuta na Gesi Baharini katika Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo.Kushoto ni Waziri wa Nishati na Madini Professa Sospeter Muhongo na kulia pembeni ya Rais ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPDC Mhandisi Joyce Kisamo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia kwenye Mkutano wa Nne wa Kugawa Vitalu vya Utafutaji Mafuta na Gesi Baharini katika Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya wajumbe walihudhuria uzinduzi wa Mkutano wa Nne wa Kugawa Vitalu vya Utafutaji Mafuta na Gesi Baharini katika Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwaeleza waandishi wa habari jinsi utafiti wa Gesi na mafuta unavyofanyika baharini muda mfupi baada ya kuzindua awamu ya nne ya Utafiti wa Gesi na mafuta uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo.Rais Kikwete aliwahi kuingoza wizara ya Nishati na Madini.Picha na Freddy Maro.

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake