Thursday, October 31, 2013

RATIBA YA KUAGA NA MAZISHI YA SPECIAL FORCE COMANDO LT. RAJAB MLIMA LEO ALHAMISI

*Saa mbili hadi tatu kuwasili (0800-0900 hrs) kwa Maafisa na Watumishi wa Umma na waombolezaji uwanja wa mpira Lugalo 521 KJ

*Saa nne na dakika tano asubuhi (1005 hrs) kuwasili Mwili wa Lt. Rajab Mlima

*Saa nne na dakika kumi hadi saa tano na dakika ishirini (1010-1120 hrs) Mgeni Rasmi kuwaongoza waombolezaji kutoa heshima zao za mwisho.
Saa tano na dakika thelathini na tano (1135 hrs) mwili wa kuondolewa Lugalo kupelekwa nyumbani Mbezi Beach.

*Saa tano na dakika arobaini na tano (1145 hrs) mwili kuwasili nyumbani Mbezi Beach.

*Saa sita mchana hadi saa nane na nusu  (1200-1430) sala ya kumuombea marehemu na chakula cha mchana.

*Saa tisa kasorobo mwili utaondoka kuelekea msikiti wa Maamur Upanga Dar Es Salaam.

*Saa kumi kamili hadi saa kumi na robo (1600-1615) sala ya Alasiri na sala ya kumuombea Marehemu.

*Saa kumi na nusu 1630 hrs mwili kuwasili Makaburi ya Kisutu na taratibu za mazishi. Na kuondoka baada ya mazishi.

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake