Waziri wa Fedha Omar Yussuf Mzee
Sherehe za utiaji saini makubaliano hayo zilifanyika leo katika Wizara ya Fedha, Vuga ambapo Waziri wa Wizara hiyo Omar Yussuf Mzee aliiwakilisha Zanzibar na Balozi mdogo wa China hapa Zanzibar Xie Yunliang aliiwakilisha nchi yake.
Akizungumza baada ya utiaji saini, Waziri wa Fedha alisema kua msaada huo utalenga katika nyanja mbali mbali ikiwemo ujenzi wa Hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani, Uchimbaji wa visima vya maji safi na salama na kupambana na mbu wa malaria katika maeneo ambayo maradhi hayo bado yapo.
Alisema kazi iliobakia hivi sasa ni kwa Idara ya Hazina kuwasiliana na wahusika ili utekelezaji wa makusudio hayo yaweze kufikiwa kwa haraka.
Nae Balozi Xie Yunliang alisema kuwa Zanzibar na China ni nchi mbili zenye uhusiano mzuri wa muda mrefu hali ambayo imeifanya kua ni rafiki wa karibu.
Alisema makubaliano hayo ni muendelezo wa misaada wanayoitowa ili kuona Zanzibar inapiga hatua katika juhudi zake za kukuza Uchumi na Maendeleo ya wananchi.
Utiaji saini makubaliano hayo ulikwenda sambamba na kukabidhiwa hati za Taa za Barabarani zinazo tumia nishati ya jua katika Manispaa ya Mji wa Zanzibar ambapo mradi huo ulifadhiliwa na Serikali ya China.
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake