Tuesday, October 29, 2013

Stori kuhusu yule shabiki Steven wa Yanga kupata dili la kuigiza

Umaarufu wake umekuja kutokana na video kadhaa ambazo zimemuonyesha kwenye mitandao na kwenye TV akililia vitu mbalimbali ikiwemo lile tukio la mechi ya Yanga na Simba ambapo Yanga ikiwa ni timu anayoishabikia ilifungwa 5, na pia tukio jingine lililompa umaarufu ni la kulia baada ya kutoswa kwenye shindano la kusaka vipaji vya muziki la BSS.
Steve ambae ni mzaliwa wa 87.8 Mbeya, akiwa tayari ameweza kusogeza sehemu ya maisha yake kutokana na pesa zaidi ya milioni 5 ambazo amezikusanya kutoka kwa watu mbalimbali ambao waliomuonea huruma kwa ushabiki wake wa machozi, amepata dili ambalo linaweza kumpa umaarufu zaidi na hata kazi nyingi baada ya kupewa nafasi ya kuigiza kwenye movie.

Mwigizaji wa longtime Tanzania Dr. Cheni amekubali kumpa Steve nafasi ya kuigiza baada ya Steve kumtuma mtu anaitwa Boaz amsaidie kumuombea kwa Dr. Cheni ili apate nafasi ya kuigiza baada ya kupita kwa waigizaji mbalimbali ambao hawakumpa ushirikiano.
Cheni anasema ‘kwangu ilikua ngumu alipokuja kuniambia ila baada ya kukaa dakika 5 nikagundua kwamba yule bwana naweza kumpa nafasi na kuamua kutunga stori ya harakaharaka ya movie inaitwa ‘Nimekubali kuolewa’ ambayo Steve atacheza kama dereva wa bodaboda ambae namchukulia mke wake alafu anaanza kulia’

Kwenye sentensi nyingine Dr. Cheni amesema movie inaanza kuchezwa soon na atamlipa pesa Steven japo mwenyewe alisema anaomba nafasi ya kuigiza haijalishi kama analipwa au la.

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake