Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania(JWTZ) linapenda kutoa taarifa ya kifo cha Luteni Rajabu Ahmed Mlima kilichotokea tarehe 27 Octoba 2013 huko Goma DRC alipokuwa anatekeleza jukumu la Ulinzi wa Amani.
Luteni Rajabu Ahmed Mlima alipigwa Risasi wakati kikundi chetu kinakwenda kukinga Raia wasidhurike na mapigano kati ya Jeshi la Serikali ya DRC na M23 katika eneo la Kiwanja ,kwenye Milima ya Gavana
MONUSCO inaandaa utaratibu wa kuleta mwili wa Marehemu na mtajulishwa taratibu za mapokezi, Kuaga mwili wa Marehemu na mazishi.
Mungu aiweke Roho ya Marehemu mahali pema Peponi. AMIN.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao Makuu ya Jeshi.
Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment