Thursday, October 31, 2013

VIONGOZI MBALIMBALI WA KISERIKALI WAMZIKA MAREHEMU BALOZI SEPETU HAPO JANA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.akisalimiana na Padri wa Kanisa Katoliki laMinara miwili Mjini Zanzibar Cosmas Amani Shayo, alipowasili katika eneo la Mazishi ya Marehemu Balozi Issac Abraham Sepetu,yaliyofanyika kijijini kwao Mbuzini Wilaya ya Magharibi Unguja jana.Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akiwa na viongozi wengine akiwemo Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DK.Mohamed Gharib Bilali,katika Mazishi ya Marehemu Balozi Issac Abraham Sepetu,yaliyofanyika kijijini kwao Mbuzini Wilaya ya Magharibi Unguja jana.Jeneza la Marehemu Balozi Issac Abraham Sepetu,likiwa limebebwa na Askari Polisi na kulifikisha katika kaburi lake yalipofanyika mazishi kijijini kwao Mbuzini Wilaya ya Magharibi Unguja jana.Padri wa Kanisa Katoliki la Minara miwili Mjini Zanzibar Cosmas Amani Shayo, akiuombea mwili wa marehemu Balozi Issac Abraham Sepetu,wakati wa mazishi yake yaliyofanyika kijijini kwao Mbuzini Wilaya ya Magharibi Unguja jana.Jeneza lenye Mwili wa Marehemu Balozi Issac Abraham Sepetu,ukitemshwa katika kaburi wakati wa mazishi yake yaliyofanyika kijijini kwao Mbuzini Wilaya ya Magharibi Unguja jana.[Picha na
Ramadhan Othman Ikulu.]

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake