ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, October 30, 2013

WAJUMBE WA BODI YA WAKURUGENZI NSSF WATEMBELEA MIRADI DAR

Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) pamoja na maofisa wa NSSF wakitembelea mradi wa Ujenzi wa Daraja la Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) pamoja na maofisa wa NSSF wakitembelea mradi wa nyumba za bei nafuu eneo la Mtoni Kijichi.
Meneja Mradi wa NSSF, Mhandisi Karim Mattaka (wa kwanza kulia waliokaa mezani) akitoa taarifa fupi kwa Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii na maofisa waandamizi wa taasisi hiyo juu ya maendeleo ya ujenzi wa daraja la Kigamboni.
kwa picha zaidni na maelezo bofya soma zaidi
Meneja Mradi wa NSSF, Mhandisi Karim Mattaka (wa kwanza kushoto) akifafanua jambo kwa Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii na maofisa waandamizi wa taasisi hiyo juu ya maendeleo ya ujenzi wa daraja la Kigamboni.
Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) pamoja na maofisa wa NSSF wakiteremka kwenye gari katika moja ya miradi ya taasisi hiyo walipotembelea jana.

Mmoja wa maofisa wa juu na mhandisi kutoka NSSF akifafanua jambo kwa wajumbe wa bodi.
Mfisa Mradi msimamizi na Msanifu wa NSSF, Deogratias Mponeja (wa kwanza kushoto) akitoa maelezo juu ya mradi wa awamu ya tatu ya ujenzi wa nyumba nafuu kwa wajumbe.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk. Ramadhan Dau (wa pili kulia) akiwa na Eunice Chiume wakizungumza jambo katika ziara ya wajumbea wa Bodi ya NSSF kutembelea miradi jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Mradi na Msanifu Majengo wa NSSF, Mkurugenzi wa Mipango, Miradi na Uwekezaji wa NSSF, Yacoub (aliyesimama) akitoa taarifa fupi juu ya maendeleo ya mradi wa ujenzi wa nyumba za bei nafuu kwa wajumbw wa bodi.
Na Joachim Mushi, Dar es Salaam

WAJUMBE wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) wamefanya ziara ya kutembelea baadhi ya miradi kadhaa inayotekelezwa na shirika hilo iliyopo jijini Dar es Salaam. Miradi iliyotembelewa katika ziara hiyo ni pamoja na ule wa ujenzi wa nyumba za bei nafuu uliopo eneo la Mtoni Kijichi na ujenzi wa Daraja la Kisasa eneo la Kigamboni.

Akitoa taarifa fupi kwa wajumbe wa bodi ya NSSF wakiwa eneo la ujenzi wa nyumba za bei nafuu na za kisasa eneo la Mtoni Kijichi, Mkurugenzi wa Mipango, Miradi na Uwekezaji wa NSSF, Yacoub Kidula alisema eneo hilo linatekelezwa kwa awamu mbili za ujenzi wa nyumba aina mbalimbali.

Alisema awamu ya pili ambayo iliendelea baada ya kukamilika ya kwanza ya ujenzi wa nyumba 85, imetekelezwa kwa ujenzi wa nyumba 215 eneo la Mtoni Kijichi mradi ambao tayari umekamilika na nyumba zimeanza kuuzwa kwa wanachama wa NSSF. Alisema nyumba 200 tayari zimekamilika huku 15 zilizosalia zikiwa katika hatua za mwisho kukamilika.

Alisema tayari Shirika hilo limeanza kutekeleza ujenzi mwingine wa awamu ya tatu utakaowezesha ujenzi wa nyumba za kisasa na bora zaidi zenye uwezo wa kuchukua familia 820 zikiwa na ghorofa moja huku zikiwa zimeboreshwa zaidi kihuduma ukilinganisha na zilizojengwa awali.

Aidha akifafanua juu ya ujenzi wa nyumba za bei nafuu zinazoendelea kujengwa na NSSF, alisema mbali na kuwa za bei ya chini zinahuduma muhimu za kijamii kama umeme, maji, mfumo mzuri wa kuifadhi maji taka, eneo la nje la ziada pamoja na vifaa vingine zikiwemo feni vyumba vyote, mfumo wa maji ya moto kwenye mabafu na sakafu ya kisasa 'tiles'.

Alisema nyumba zinazojengwa zinaukubwa na idadi ya vyumba tofauti kulingana na maitaji ya mteja, yaani kuanzia vyumba viwili hadi vitatu vya kulala huku vyote vikiwa na sebule, jiko, choo pamoja na stoo. Aliongeza kuwa milango na madirisha yamejengwa kwa vioo na chuma (nondo) ili kuimarisha zaidi kiusalama huku jiko likiwa na kabati maalumu na za kisasa kwa ajili ya kuifadhia vitu.

Kidula alisema nyumba ya chini itauzwa takribani sh milioni 66 za kitanzania bei hiyo ikiwa ni pamoja na VAT. Wajumbe wa bodi pia walitembelea mradi mkubwa wa NSSF wa ujenzi wa daraja la Kigamboni ambao unafanywa na taasisi hiyo kwa kushirikiana na Serikali.

Akitoa taarifa za maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo, Meneja Mradi huo, Mhandisi Karim Mattaka alisema licha ya ujenzi huo kuendelea vizuri kwa sasa zipo changamoto kadhaa za ujenzi ambazo zilijitokeza hivyo kushughulikiwa mara moja.

Alisema daraja hilo la kisasa litakalokuwa na njia (barabara sita) yaani tatu za kwenda Kigamboni na tatu za kurudi linatarajiwa kuunganishwa kisasa na barabara ya Mandela huku likiwa na njia za kutosha kuzuia msongamano wa magari.

Akizungumzia ziara hiyo ya Wajumbe wa Bodi, Meneja Uhusiano Kiongozi, Huduma kwa Wateja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume alisema ni ziara ya kawaida ya wajumbe hao kukagua miradi ya taasisi hiyo na huenda ziara hiyo ikawa na manufaa ya punguzo la riba kwa wanachama wanunuzi wa nyumba hizo.
*Imeandaliwa na www.thehabari.com

No comments: